Rais wa Soka Sudan Kusini kuwania nafasi ya juu CECAFA

0
12

Rais wa Chama Cha Soka cha Sudan Kusini (SSFA) Francis, Paul Amin ametangaza rasmi kuwania nafasi ya Umakamu wa Urais wa Baraza la Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati (CECAFA).

Advertisement

Amin amekuwa akipigiwa upatu na baadhi ya Wadau wa Soka wa ukanda wa CECAFA kuwania uongozi kwenye Baraza hilo kutokana na mipango yake mizuri ya kuboresha soka nchini mwake.

Soka la Sudan Kusini kwa siku za hivi karibuni limepiga hatua kubwa kutokana na mipango na mikakati mizuri anayoifanya Kiongozi huyo, na hicho ndicho kitu kikubwa kilichowashawishi baadhi ya Viongozi wa Soka wa ukanda wa CECAFA kumtaka aingie ndani ya Baraza hilo.

Uchaguzi mkuu wa CECAFA utafanyika Disemba 18 mwaka huu huu katika jiji la Kampala nchini Uganda.Facebook Comments