Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter alazwa tena hospitali

0
5

Rais wa zamani wa Marekani, Jimmy Carter amelazwa tena hospitalini kwa kusumbuliwa na maambukizi ya njia ya mkojo.

Rais huyo mwenye umri wa miaka 95 alilazwa katika Kituo cha Matibabu cha Phoebe Sumter huko Marekani, kusini mashariki mwa jimbo la Georgia, mwishoni mwa wiki iliyopita kwa matibabu zaidi.

“Anajihisi vizuri na anatarajia kurudi nyumbani hivi karibuni,” taarifa hiyo ilisema.

Rais huyo wa 39 wa Marekani aliyeiongoza nchi hiyo kati ya 1977 na 1981 alisimamia kuhalalisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Marekani na China miaka 40 iliyopita.