Rasmi: Selemani Matola aachana na Polisi Tanzania

0
11

Uongozi wa Klabu ya Polisi Tanzania umethibitisha kuachana na kocha wake Msaidizi Selemani Matola ambaye amepata ajira katika timu nyingine.

Akizungumza Azam Sports, Msemaji wa Polisi Tanzania, Frank Geofrey amesema wameachana na Matola bila tatizo lolote na wamemtakia kila la kheri katika maisha yake mapya

Geofrey amesema hawatatafuta kocha msaidizi mwingine, kwani Kocha Mkuu Ally Mtuli atasaidiana na kocha wa viungo katika kuiongoza timu.