RC Ayoub azindua huduma ya mama na mtoto Umbuji

0
6

Na Thabit Madai,Zanzibar.

Mkuu wa mkoa wa kusini Unguja  Ayoub Mohammed Mahmoud azindua huduma za mama na mtoto katika kituo cha afya Umbuji.

Akizungumza mara baada ya uzinduzi huo amesema kuzinduliwa kwa huduma hizo kutawasaidia wakaazi wa Umbuji na vitongoji vya jirani ili kuhakikisha wanapata kujifungulia katika kituo hicho.

Amesema awalikulikuwa na huduma za mama na motto zikihusisha upimaji wa uzito na ujauzito pekee hivyo kuzinduliwa kwa kituo hicho kitawasaitia wananchi wa kijiji hicho kutokutumia masafa marefu kwa ajili ya kujifungua.

Aidha amesema kuchelewa kwa ufunguzi wa kituo hicho kulitokana na uhaba wa watendaji wakiwemo maafisa tabibu pamoja na vifaa yambo ambalo lilipelekea washindwe kufungua huduma hizo.

Hata hivyo Ayoub amewataka wananchi kutumia njia sahihi katika kuwasilisha malalamiko yao na siyo tu kukimbilia katika vyombo vya habari na badala yake wazifishe kwenye serikali kwa ngazi hadi ngazi.

Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa kituo hicho mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya kati ngugu, Mohammed S. Mohammed amesema kuwa atahakikisha kuwa wafanyakazi wanakuwemo wakutosha,upatikanaji wa huduma bora sambamba na usalama wa wananchi kutokana na huduma wanazopatiwa na uwepo wa madawa yanayotolewa bure.

Kwa upande wa wananchi wamesema kuzinduliwa kwa kituo hicho kutawaondoshea kwa kiasi kikubwa adha ya kuifata huduma hiyo sehemu za mbali.

Kituo hicho cha mama na motto Umbuji kimejengwa na serikali kupitia mradi wa Orio wenye lengo la kutoa huduma za mama na motto pamoja na kujifungulia ili kuhakikisha wapunguza msongamano wa wazazi katika hospitali kuu ya Mnazi Mmoja.