TATIZO LA KIFAFA CHA MIMBA

0
19

Kifafa cha mimba (Eclampsia)

Kifafa cha mimba (eclampsia) ni matokeo ya ugonjwa wa pre eclampsia.

Pre eclampsia

ni pale ambapo mama mjamzito anakuwa na blood pressure ambayo ni kubwa kuliko kawaida(zaidi ya 140/90) na kuongezeka na protini kwenye mkojo.Hii huendana na dalili zingine kama:-

 -maumivu makali ya kichwa,

-kuvimba miguu

– Kuwa na uzito mkubwa (obesity/over weight)

-maumivu ya chembe moyo(epigastric pain),

-kushindwa kuona vizuri(blurred vision),

-Kupungua kwa Mapigo ya moyo ya mtoto

-Kutokukua kwa mtoto tumboni(intra uterine growth restriction)

Eclampsia (kifafa cha mimba)

Hali hii hutokea pale ambapo pressure inaendelea kupanda bila kuchukuliwa hatua au msaada wowote,

-Mama hupata Seizures/convulsions(degedege/kifafa)

-Mama huweza kuchanganyikiwa(confusion),

-Mama huweza kupoteza fahamu(loss of consciousness).

Sasa zinapotokea dalili kama (degedege/seizure na kuchanganyikiwa) ndipo tunasema mama ana kifafa cha mimba.

wakati wakutokea kwa kifafa cha mimba

Pre eclampsia na kifafa cha mimba (eclampsia)hutokea mara nyingi kuanzia wiki ya 24, na pia baada ya kujifungua. Mara chache pia inaweza kutokea kabla ya wiki 24.

Sababu zinazopelekea mama mjamzito kupata kifafa cha mimba

Chanzo cha huu ugonjwa bado haijulikani ni nini, lakini kuna baadhi ya mambo ambayo yatakayo kuweka hatarini kupata kifafa cha mimba navyo ni:-

-Ujauzito wakwanza kwa mama

-Kuwa na  historia ya eclampsia katika familia upande wako.

-Mara nyingi wanawake wajawazito wenye chini ya miaka 20 au zaidi ya miaka 40 wapo katika hatari kubwa ya kupata kifafa cha mimba.

-Kama Mama alikua na tatizo la high blood pressure kabla ya ujauzito.

-Kuwa na uzito mkubwa kulingana na urefu wako(overweight/obesity).

-Kuwa na  historia ya kifafa cha mimba katika ujauzito uliopita.

-Muda kati ya mimba. Kuwa na watoto chini ya miaka miwili au zaidi ya miaka 10 mbali husababisha hatari kubwa ya preeclampsia.

-Mama mwenye mimba  ya mapacha au zaidi ya wawili.

-Kama baba wa ujauzito huo ni mpya tofauti na wa ujauzito wa awali nao huwa katika hatari yakupata  kifafa cha mimba.

Ingawaje hakuna kinga ya uhakika ya kifafa cha mimba

 Sasa wanawake walio kwenye makundi ambayo yapo katika hatari na uwezekano mkubwa wa kupata kifafa cha mimba wanaweza kujikinga kwa kutumia vidonge vya aspirin na madini ya calcium. Lakini  Kabla ya kutumia dawa hizi ni muhimu kupata ushauri wa kitaalam.

-Na tiba pekee ya kifafa cha mimba ni kumzalisha mjamzito. Hii ni kwa sababu kifafa cha mimba husababishwa na kuwepo kwa kondo la nyuma ndani ya tumbo la  uzazi.  Hivyo basi bila kutoa kondo la nyuma Mama hawezi kuwa Sawa.

-Iwapo Mama mjamzito atagundulika kuwa ana kifafa cha mimba  kabla mtoto hajakomaa na kuwa tayari kwa kuzaliwa.

Daktari anaweza kushauri mjamzito alazwe na kuangaliwa kwa ukaribu wakati ikisubiriwa kukomaa kwa mtoto. Vilevile daktari anaweza kushauri mjamzito apewe dawa ya kuharakisha kukomaa mapafu ya mtoto.

Iwapo hali ya mjamzito ikibadilika na kuwa mbaya, kuzalishwa kunaweza kuwa ni lazima hata kama mtoto hajakomaa kwa sababu kuna hatari kubwa ya kumpoteza mama na mtoto iwapo ujauzito utaendelea.

Hatari zinazoweza kutokea iwapo ujauzito utaachwa uendelee

 -mtoto kufia tumboni.

-Mama mjamzito huweza kupoteza uwezo wa kuganda kwa damu na kusababisha mjamzito kupoteza damu nyingi wakati wakujifungua.

-kondo la nyuma kujitenga na tumbo la uzazi kabla ya mtoto kuzaliwa,

– Kuharibika kwa baadhi ya ogani za mjamzito kama digo kushindwa kabisa kufanya kazi.

-Mama mjamzito upata kiharusi (stroke) au mjamzito kupoteza maisha.

Kwenye kumzalisha mama mwenye kifafa cha mimba njia mbalimbali huweza kutumika kutegemeana na hali ya mjamzito. Kama hali sio mbaya sana na njia ya uzazi imeshaanza kufunguka, mjamzito anaweza kupewa dawa za kuanzisha uchungu na kujifungua kwa njia ya kawaida.

Kujifungua kwa njia ya operesheni hulazimika kwa wajawazito wenye msukumo mkubwa sana wa damu na wale ambao hali zao sio nzuri au kunapokuwepo na sababu nyingine ya kujifungua kwa operesheni.

Kabla ya kujifungua, mjamzito mwenye msukumo mkubwa wa damu hupewa dawa za kupunguza msukumo wa damu.

Ili kuzuia uwezekano wa kupata “degedege“, daktari anaweza kushauri mgonjwa apewe madini ya magnesium kwa njia ya dripu.

Kwa sababu ugonjwa wa kifafa cha mimba huongeza uwezekano wa damu kuganda mwilini, daktari anaweza kushauri mgonjwa atumie dawa ya kuzuia damu kuganda.

Baada ya kujifungua, msukumo wa damu unategemewa kurudi kwenye hali yake ya kawaida katika muda wa masaa 24. Hata hivyo ni vizuri mama aliyejifungua katika hali hii kuangaliwa kwa masaa 48 kabla hajaruhusiwa kwenda nyumbani.

Kwa vile upo uwezekano wa msukumo wa damu kuendelea kuwa juu moja kwa moja. Mzazi hushauriwa kupima msukumo wa damu mara kwa mara, iwapo baada ya wiki sita (siku 40) itaonekana msukumo wa damu unaendelea kuwa juu, basi hushauriwa kuendelea na matibabu ya msukumo mkubwa wa damu kama wagonjwa wengine wenye ugonjwa wa msukumo mkubwa wa damu.

Ni vyema mama mjamzito kuhudhuria kliniki kwa wakati na kuangaliwa kwa umakini na kufanyiwa vipimo stahiki kulingana na huduma anazotakiwa kuzipata ili kugundua tatizo mapema na kuweza kumsaidia atakaye kutwa na tatizo hilo.