Utalii wa kanda ya ziwa kutangwaza

0
5

Rais wa Chemba ya Biashara, Viwanda na Kilimo (TCCIA) Paul Koyi amesema kuanzishwa shughuli za kutangaza Utalii wa Kanda ya Ziwa kutasaidia kukuza Uchumi wa wananchi wa Kanda ya Ziwa, Tanzania na Afrika mashariki kwa ujumla.

Akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Tovuti ya L-VIC Investment Limited yenye lengo la kutangaza vivutio vya Utalii Kanda ya Ziwa Koyi amesema ni asilimia 12 tu ya Biashara ndiyo hufanyika baina ya wananchi huku Biashara zote asilimia 70 zikifanyika nje ya a nchi Jambo ambalo litapungua kupitia shughuli za Utalii wa Ziwa Victoria.