Waendeshsaji pikipiki Rwanda kutumia mita maalum

0
6

Watu wanaofanya biashara ya kubeba abiria kwa kutumia pikipiki nchini Rwanda wametakiwa kuanza kutumia mita maalum ya kupima muda ya kulipisha wateja wao.

Waendeshaji hao wa pikipiki wamepewa hadi Julai mwaka kesho kuaza kutumia mita hizo. Rwanda ina zaidi ya wanedeshaji pikipiki 36,000.

Tayari baaadhi ya wadau wameanza kujisajili ili kutumia mita hizo ambazo pia zitapunguza matumizi ya pesa taslim wakati wa ulipaji.

Mita hizo zitauzwa na kampuni za Pascal Technology Ltd Rwanda na Altron, ya Afrika Kusini ambazo tayari zimetiasaini makubaliano ya kuwekeza dola milioni 18.