Watu 30 wahofiwa kufariki katika matope nchini Uganda

0
6

Zaidi ya watu 30 wa Wilaya ya Bududa iliyopo Uganda Mashariki wamehofiwa kufariki kutokana na kufukiwa na matope yaliyosababishwa na mafuriko yaliyotokea katika eneo hilo kufuatia mvua kubwa ya saa tano mfululizo.

Advertisement

Mafuriko hayo yamesababisha kukithiri kwa matope katika vijiji vya vijiji vya Namasa na Naposhi, vinavyopatikana katika Kaunti ndogo ya Bushika.

Mafuriko hayo yaliripotiwa kuingia katika nyumba zaidi ya 20, mashambani na kusababisha Barabara nyingi wilayani hiyo kujaa maji jambo lililosababisha harakati za uokoaji kuwa ngumu.

Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa kijiji cha Namali Bwana Moses Lukuya, alisisitiza maji yamefurika kiasi ambacho hawawezi kuvuka kwenda nyumbani wakitokea kazini.

Kamanda wa Polisi wa Wilaya ya Bududa alituma timu kusaidia katika juhudi za uokoaji, maafisa wameshindwa kuvuka kwenye maeneo yaliyoathirika kwa sababu barabara hazipitiki.

Diwani wa Kata ya Bushika, Bwana Simuya Mabuko aliiomba serikali kuwahamisha watu kutoka katika maeneo yaliyoathirika na matope wilayani hapo.

Mwaka jana, zaidi ya watu 850 walihamishwa makazi yao na wengine 51 walikufa, kutokana na mafuriko na matope yaliyozikumba kaunti za Bukalasi na Buwali wilayani Bududa. Maeneo hayo pia yaliguswa na mmomonyoko mwingine wa ardhi mnamo Juni mwaka huu, ambao uliwaacha watu wasiokufa watatu.Facebook Comments