Wizara ya Elimu yatoa Bilioni 2 kwa Chuo hiki

0
8

Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia itatoa kiasi cha Shilingi Bilioni mbili kwa ajili ya kuanza ujenzi wa Ndaki ya Afya na Sayansi Shirikishi ya Chuo Kikuu Dar es Salaam iliyopo Mbeya.

Hayo yamesemwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako alipofanya ziara katika Ndaki hiyo jijini Mbeya Desemba 2, 2019.

Ndalichako amesema ni vema ujenzi wa Chuo hicho ukaanza mara moja baada ya kupata eneo ili kuondoa changamoto ya vyumba vya madarasa kwani kwa sasa wanafunzi wamekuwa wengi katika Ndaki hiyo na hivyo kushindwa kutoa mafunzo kwa ufasaha.

Ndalichako amesema Serikali ya Awamu ya Tano imefanya uwekezaji mkubwa kwenye sekta ya Afya kwa kujenga vituo vya afya na imeendelea kuimarisha hospitali za Rufaa na zile za Wilaya hivyo uhitaji wa madaktari wa kuweza kufanya kazi katika maeneo hayo kuongezeka.

 Uanzishaji wa Ndaki hiyo katika Hospitali ya Rufaa Mbeya ni mkakati mmojawapo wa kuongeza fursa za utoaji Shahada za udaktari kwa watimu wenye ufaulu unawawezesha kudahiliwa katika programu hiyo.

“Niwaakikishie kwamba Serikali imeshaamua kuongeza nafasi za udahili katika program za afya Chuo Kikuu cha Dar es salaam hapa Mbeya (MCHAS) na pia katika Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Muhimbili (MUHAS).