ZECO watoa mchango kwa Zanzibar Heroes

0
9

Na Thabit Madai,Zanzibar.

Shirika la Umeme Zanzibar (ZECO) limetoa mchango wa Shilingi million Moja kwa kamati ya Hamasa ya timu ya Taifa ya Zanzibar heroes ambayo inatarajiwa kusafiri kesho kuelekea Nchini Uganda katika    Mashindano ya Cecafa Seniors Challenge Cup.

Akikabidhi Mchango huo Afisa Habari na Uhusiano wa Shirika la Umeme Zeco, Salum Abdallah alisema Zeco wametoa mchango huo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za wadau wa michezo katika timu hiyo.

“Tumetoa kiasi hichi kidogo katika kufanikisha Timu hii  yetu iweze kusafiri kwenda Uganda na kurudi na ubingwa”alisema Afisa huyo.

Katika maelezo yake aliwaomba mashirika mengine kuweza kujitokeza kuchangia timu hiyo.

“kutoa n moyo si utajiri, tunaomba wadau wengine wakiwa ikiwemo mashirika mengine ya Serikali kutoa michango yao kwa timu hii ya Taifa ya Zanzibar”alisema Afisa huyo.

Nae Mwenyekiti wa kamati hiyo Ayoub Mohamed Mahmoud alisema pongeza wadau mbali mbali ambao wanajitokeza kutoa misaada kwa timu hiyo ya Taifa.

Alisema kuwa kwa siku ya leo tayri wameshapokea shilingi Milion tano kutoka kwa kampuni ya Penny royal pamoja na Baraza la Wawaklishi Milion nane.

“Tunashukuru kwa wadau wengi kujitokeza na kuwa na hamasa katika  kutoa mchango kwa timu yao ya taifa , Tumepokea million nane kutoka baraza la wawakilishi na million Tano kutoka Penny royal na hwa wametupa million moja” alisema Ayoub ambaye pia mkuu wa mkoa wa kusin unguja.

Mashindano hayo yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi tarehe 07 mwezi huu huku Zanzibar heroes ikianza mashindano hayo kwa mchezo wa kwanza na ndugu zao Kilimanjaro stars.