Australia yatangaza hali ya dharura

0
3

Maafisa nchini Australia leo wametangaza hali ya dharura katika eneo linalojumuisha mji mkuu wa Canberra huku moto wa kichakani ukitishia kusambaa zaidi kutokana na joto pamoja na upepo mkali.

Tamko hilo ni la kwanza la aina yake katika ene hilo tangu moto wa mwaka 2003 ulioteketeza zaidi ya theluthi mbili ya eneo lote la ardhi, na kusababisha vifo vya watu wanne na kuharibu nyumba 470.

Moto huo kwa sasa umeathiri hekta 185,500, sawa na asilimia 8 ya jumla ya eneo hilo. Hali hiyo ya dharura ambayo itadumu kwa masaa 72, itatoa muda wa kuhamisha watu, kufunga barabara na kuzinusuru nyumba za watu binafsi.

Facebook Comments