Baba wa Samata: Ndoto yetu na Mbwana ilikuwa ni kucheza ligi kuu ya Uingereza

0
23

Baba wa nahodha wa Tanzania Mbwana Samata anajivunia mafanikio ya mtoto wake katika ulimwengu wa kandanda na kusema kuwa siku zote yeye na mwanaye walikua wanatamani acheze kwenye ligi kuu ya uingereza.

Ndoto hiyo inakaribia kukamilika wakati huu ambapo Aston Villa inatumai kukamilisha makubaliano ya dau la £10m kumsajili mshambuliaji huyo wa klabu ya Genk ya Ubelgiji.

”Siku anacheza na liverpool nilisema akiwafunga nitamchinjia jogoo nilifurahi sana hata sasa ndoto imetimia tulikua tuna ndoto ya kutua uingeleza kwakua ndio ligi pendwa kwa sasa” alisema baba mzazi wa Samatta

Facebook Comments