China yaahidi kuudhibiti mlipuko wa corona

0
4

China imesema leo kwamba ina imani kwamba itaweza kuudhibiti mripuko wa homa inayotokana na virusi vya corona huku idadi ya visa vilivyothibitishwa ikikaribia watu 10,000 duniani kote.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje Hua Chunying amewaambia waandishi habari kwamba China itafanikiwa kubambana na changamoto zinazotokana na virusi hivyo vilivyoanzia nchini humo mnamo mwezi Desemba.

Ameongeza kwamba China inashirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) ambalo limeutangaza mripuko huwa kuwa dharura ya afya ya kimataifa. Hadi jana usiku, China imethibitisha vifo 213 vinavyotokana na homa ya virusi hivyo vya corona.

Kulingana na WHO hamna mtu aliyefariki katika nchi nyingine licha ya kurekodiwa visa 98 duniani kote.

Facebook Comments