Corona yagonga hodi Uingereza, wawili wathibitishwa kuwa na virusi hivyo

0
4

Watu wawili wamegundulika kuwa na virusi vya corona nchini Uingereza, mkuu wa idara ya afya nchini humo ametangaza.

Takriban watu 213 nchini china wamepoteza maisha kutokana na virusi hivyo, hasa kutoka mjini Hubei, huku kukielezwa kuwa na watu 10,000 walioathirika nchi nzima.

Watu 98 wamegundulika kuwa na virusi katika nchi nyingine 18.

Shirika la afya duniani limetangaza mlipuko wa virusi vya corona ni janga duniani.

Kwa sasa, raia 83 wa Uingereza na 27 wa mataifa ya kigeni wanarejea Uingereza kutokea Wuhan, mji ambao ni kitovu cha mlipuko nchini China.

Advertisements

Abiria hao watawekwa karantini katika hospitali ya Arrowe Park kwa majuma mawili.

Profesa Chris Whitty , afisa mkuu wa matibabu nchini England alisema: Idara ya afya nchini Uingereza imejiandaa vya kutosha na ina uzoefu wa kuzuia maambukizi na tayari tunafanya kazi mara kwa mara kutambua wale waliokaribiwa na wagonjwa ili kuzuia maambukizi zaidi.

Tumejiandaa kuzuia visa vya Uingereza vya ugonjwa wa virusi vya Corona na tuna njia nyingi za dharura kukabiliana na virusi hivyo, aliongezea.

Profesa Whitty alisema kwamba Uingereza inafanya kazi kwa karibu na shirika la Afya duniani WHO pamoja na jamii ya kimataifa huku mlipuko huo nchini China ukiendelea ili kuhakihs akuwa tuko tayari kwa lolote litakalotokea.

Facebook Comments