Familia yashtaki baada ya kuondolewa katika ndege kwa madai ya kunuka ‘harufu mbaya’

0
7

Familia moja ya Michigan iliotolewa katika ndege moja mjini Miami baada ya wafanyakazi wa ndege hiyo kusema wananuka harufu mbaya sasa wameamua kuishtaki kampuni hiyo ya ndege.

Yehuda Yosef Adler, mkewe Jennie na mwana wao wa kike walitimuliwa kutoka katika ndege hiyo iliokuwa ikilekea Detroit Januari iliopita.

Advertisements

Wanasema kwamba wafanyakazi walizungumzia kuhusu dini yao ya kiyahudi. Kampuni ya American Airline imesema kwamba uamuzi wa kuindoa familia hiyo haukutokana na dini yao.

Inadaiwa kwamba wateja walilalama kuhusu harufu ya bwana Adler. Kesi hiyo iliowasilishwa mjini Texas , inadai hatua hiyo ilimuharibia jina , kumfanya awe na huzuni na kumbagua kidini.

Bwana Adler anadai kwamba familia yake ilikuwa tayari imeketi katika viti vya ndege hiyo kwa zaidi ya dakika tano wakati mfanyakazi wa ndege alipowaambia kwamba kuna dharura na kwamba walihitajika kuondoka katika ndege hiyo.

Wakati walipoondoka katika ndege hiyo , bwana Adler anadai kwamba wafanyakazi walikuwa wakiwaondoa katika ndege hiyo kutokana na harufu mbaya ya mwilini waliokuwa nayo.

Kesi hiyo inasema kwamba mfanyakazi mmoja alitoa matamshi mabaya, akiambia familia hiyo kwamba anajua Wayahudi wa kiothodoksi huoga mara moja kwa wiki.

Familia ya Adler baadaye iliwafuata watu katika lango la ndege hiyo na kuwauliza iwapo wananuka harufu mbaya.

Wanasema kwamba waliwauliza watu 20 lakini hakuna mmoja aliyesema kwamba atahisi harufu mabaya. Bwana Adler pia alisema kwamba walioga walipoamka alfajiri hiyo.

Walipatiwa chumba cha hoteli na chakula na wakawekwa katika ndege nyengine iliokuwa ikielekea Detroit asubuhi iliofuata .. lakini walikuwa bila mizigo yao kwa kuwa haikutolewa kutoka katika ndege hiyo ya kwanza.

Taarifa kutoka kampuni hiyo ya ndege iliotolewa kwa runinga ya Fox News ilisema: Familia ya Adler ilitakiwa kushuka katika ndege baada ya abiria kadhaa na wafanyakazi kulalamika kuhusu harufu mbaya ya bwana Adler na kwamba uamuzi huo ulifanywa kutokana na wasiwasi wa wateja wetu.

”Uamuzi uliochukuliwa haukutaja kuhusu dini ya Adler”.

Facebook Comments