Fid Q kudondosha show ya nguvu Tamasha la Kan Festival

0
9

Na Ferdinand Shayo,Arusha.

Msanii  Hodari wa Miondoko ya Hip Hop nchini Fareed Kubanda (Fid Q) anatarajia kufanya show ya kali ya kimataifa katika Tamasha la sanaa la Kimataifa la KAN Ferstival litakalofanyika  eneo la Usa River ambapo tamasha hilo litaanza january 22 hadi 25 mwaka huu.

Mkurugenzi wa sanaa katika Tamasha hilo Dave  Ojay amesema kuwa Tamasha hilo linalenga kuhamasisha sanaa ya Kiafrika ,Utamaduni wa Kiafrika ambapo Wasanii mbalimbali watatumbuiza akiwemo Msanii Mahiri Fid Q.

Licha ya Msanii huyo kuwepo kutakua na wasanii wa Isabella  Novella kutoka  Msumbiji  ,Tear Drop kutoka Kenya,na Victor Kunonga kutoka Zimbabwe  pamoja na Wachekeshaji  na Live Band.

Mkurugenzi wa Programu katika kituo  cha Mafunzo ya Uongozi  ambacho ni cha Ushirikiano wa Denmark na Tanzania  (MS-TCDC)  MSTDC ,Sara Ezra Teri  hi limelenga katika kusaidia kubadilishana ujuzi mbalimbali ikiwemo sanaa pia kuwaelimisha vijana , pia jinsi ya kuzikabili changamoto mbalimbali ikiwemo mimba za  utoto,ukosefu wa ajira,rushwa na ufisadi.

Advertisements

Sara amewataka vijana kujitokea kwa wingi katika Tamasha hilo na kutumia fursa za mafunzo yanayotolewa na kituo hicho katika kujiendeleza kielimu.

Facebook Comments