Health je Mafuta ya Nazi na Mafuta mengine Yenye Asili...

je Mafuta ya Nazi na Mafuta mengine Yenye Asili ya Mgando yanaongeza Lehemu (cholesterol) mbaya kwenye damu?

-

Professor Harvard: Mafuta ya Nazi ni Sumu, Yanaongeza Cholestrol mbaya kwenye damu LDL-C na kusababisha magonjwa ya moyo.  Katika video yake Imezua Gumzo kubwa sana Duniani ila Yawezekana ni Mtizamo wake Binafsi sio La Jopo la Wanasayansi Wote duniani.
“Kwa mujibu wa Mwongozo wa Lishe mwaka 2015-2020 Ukomo au Kizuizi cha kiwango cha Cholestrol kwa siku 300mg Umeondolewa”
Kwa miaka zaidi ya 35 tuliaminishwa “Cholestrol ni hatari kiafya usizidishe gram 300 kwa siku. Ila sasa Ukomo Umeondolewa katika mwongozo Mpya wa amerika. Umesema “Tumeamua kuondoa ukomo wa cholestrol”  Ni jambo la kushangaza  na haileti maana kisayansi Ünaondoa Ukomo wa kitu ambacho kimekuwa kikitizamwa kama sumu kwa miaka mingi Zaidi ya 35”
Hebu Jiulize Kitu ambacho ni Hatari kwa afya tumepigwa soga wee wee, Tumetengeneza dawa za kushusha cholestrol weee,Tumebadilisha vyakula vikaitwa low fat,Skimmed milk,Cholestrol free,Lean meat, egg white,Skinless chicken mwisho wa siku wanaondoa UKOMO. Nini Maana yake?  Maana ni kuwa “Walifanya makosa kuhusianisha mafuta Yanayoganda na magonjwa ya moyo”
UKWELI UMEANZA KUJIDHIHIRISHA KWAMBA “CHOLESTROL SIO KIHATARISHI NA WALA KISABABISHI CHA MAGONJWA YA MOYO” Ipo Siku Dunia nzima Itatikisika na Viwanda Vitatikiswa siku wakisema waziwazi juu ya jambo zito kama hili, Kuondolewa kwa ukomo wa kiwango cha cholesterol kwa siku ni habari njema sana kwetu tunaopigania kuboresha afya za mamilioni ya watu wanao angamia kwa kukosa maarifa..
Najua hata wewe HUJAUSOMA MWONGOZO WA LISHE KASOME UONE INGIA GOOGLE UTAFUTE NA USOME WOTE. Mtanzania Anakabidhi Maisha yake kwa Kutokuwa na Tabia ya kujisomea hata vitu vidogo vidogo kama Hivi. Be concerned na afya yako Hakika hutaugua hovyo hovyo Magonjwa yanayo Epukika. Mwongozo wa Lishe 2015-2020
Ndio Huyu Profesa anaendelea na Kusimamia Kile ambacho KIMESHA KUWA PROVEN WRONG.
Katika Video hio inayo sambaa huyo Daktari kasema kwamba “Mafuta ya nazi yanaongeza LDL-C kitalamu ni kibebeo cha cholestrol ambacho hupeleka cholestrol kwenda kwenye mishipa ya damu. Na kwa hio kazi yake LDL-C nyingi huhusishwa na Uhatari wa magonjwa ya moyo.
Ingawaje Tafiti ya kimaabara iliyofanyika kwa kuwatenga watu katika makundi matatu na kuwapa mafuta ya nazi mzeituni na Siagi (Butter) gram 50 kwa muda wa wiki kadhaa chakushangaza ni kwamba Uwezo wa Mafuta ya nazi gram 50 na mafuta ya Olive oil gram 50 katika kupandisha LDL-C inayo husishwa na uhatari wa magonjwa ya moyo Effect yake ilionekana ni sawa hakuna utofauti.
Mbali na hivyo Tafiti iliyofanywa na Prof Uffe  Ravnskov mtafiti na Mbobevu wa Cholestrol alitizama Vipimo vya tafiti zilizojumuisha watu milion 2 kuangalia kama kuna uhusiano kati ya LDL-C na Magonjwa ya Moyo kwa watu wazima. Kilicho mshangaza “Hakuna Uhusiano na Tafiti ilionesha kinyume chake” Kwamba waliokuwa na LDL-C Nyingi Walionekana kuishi Umri mrefu. 
Mbali na Hivyo Nazi Inaongeza HDL-C ambayo wengi tunaita kwa jina maarufu kama cholestrol nzuri.
Harvard bado Wanatumia Nguvu nyingi sana Kupotosha Jamii vitu vingine Vimegonga mwamba “Tafiti anayo husianisha kwamba nazi Huongeza LDL-C ambayo ndio wengi huita cholestrol mbaya zimekanushwa na Tafiti nyingi.
Tafiti niliyo ambatanisha inaonesha “Olive oil ina uwezo sawa na Nazi kwenye kupandisha LDL” Kwa hio Uhusiano huo Hauna maana yoyote. Kwa maana hio hata Olive oil nayo kwa sababu Tafiti za maabara zinasema ina uwezo sawa nayo ni mabaya?
Kama hoja ni kwamba Mafuta yanayo ganda ndani ya nazi ndio ubaya wa nazi, Hilo lishapingwa vikali kutokana na Mapungufu ya Mwongozo wa Lishe wa mwaka 1977.
Soma Mtafiti aliyejikita kutafiti mwongozo wa lishe jinsi alivyokosa Ushawahidi wa kutosha kwa nini Mafuta yanayo ganda ni hatari kwa binadamu wakati maisha ya enzi kabla ya mafuta ya mimea yalitumika na tulikuwa ndiyo sehemu ya Lishe ya babu na bibi zetu.
Soma Hapa zaidi:
  1. Tafiti za kimaabara zilizotumika kuunda mwongozo wa Lishe nazo hazikuonesha ushahidi kwamba “mafuta yanayo ganda kutoka kwenye vyakula tunavyokula ni hatari”. Pia rejea za kitafiti zinaonesha kwamba mtafiti aliye husisha mafuta yanayoganda na magonjwa ya moyo alitumia mafuta yanayoganda ya mbegu za mimea (Margarine) na sio mafuta ya wanyama na nazi.
Tafiti mbalimbali za marejeo zinaonesha kwamba hakukuwa na ushahidi wa kutosha kupitisha mwongozo unao zuia vyakula vyenye mafuta mgando na kuhusishwa kwake kusababisha magonjwa ya moyo hakukuwa na hoja za kitafiti toshelevu. Tafiti zote za Kimaabara zimeshindwa kuhakiki kwamba kama ni kweli mafuta yanayo ganda kutoka kwenye vyakula yanasababisha magonjwa ya moyo.
  1. Mbali na hivyo tafiti za kutumia watu zilizofanyika nje ya maabara nazo zimegoma kuonesha ushahidi wa kutosha kwamba mafuta ya wanyama na nazi au yanayoganda kutoka kwenye vyakula asili yanasababisha magonjwa ya moyo.
  1. Mbali na hivyo Profesa na Mtafiti makini Zoe Harcombe aliyebobea katika historia ya sayansi ya kuundwa kwa mwongozo wa lishe wa kwanza mwaka 1977. Aliweza kufanya marejeo ya tafiti mbalimbali zote nyuma na hadi sasa kutaka kuona kama mwongozo wa lishe unaokataza mafuta ya vyakula yenye asili ya kuganda kama kuna ushahidi wa kutosha kisayansi. Kwa mshangao mkubwa hakuna Ushahidi wa kutosha kwamba mwongozo huo uliundwa kwa kutumia hoja za kisayansi na hivyo basi ni batili na anaungana na wanasayansi wengine duniani kote kudai mwongozo ufanyiwe mapitio upya na ubadilishwe kwani kwa sasa unaumiza afya ya walaji wanao ufuata mwongozo huo.
  1. Mwandishi mashuhuri wa habari za Kisayansi na mtafiti Nina Techoiz alifanya marejeo ya tafiti zote za Mwongozo wa lishe “Mafuta yanayoganda ni mabaya, Mafuta ya alizeti pamba soya mahindi ni mazuri, Wanga asilimia 55-60” Kilicho mshangaza Hakuna ushahidi wakutosha kuhusu Mapendekezo hayo yote. 
Kwa Hio Kama mafuta ya nazi “Ubaya wake ni kwamba mafuta yanaganda hilo kitafiti limekanushwa vyakutosha na Hakuna ukweli wowote kwamba mafuta yanayoganda husababisha magonjwa ya moyo”
Unatakiwa Utambue kwamba tafiti za afya au zozote sio Mashindano ya mpira kwamba mwenye Point nyingi ndiye anayeshinda. Hapana hata kama kuna Tafiti moja Inakinzana na hypothesis yako Unatakiwa kurudia tena. Ndio maana Tafiti kubwa duniani zimejaribu kuhakiki na kutuaminisha “Saturated fat is bad zimeishia kupoteza pesa na zimeshindwa”
Nimeandika historia ya kuibuka kwa mafuta ya mbegu za mimea na kwa nini mafuta salama ya mgando ikiwemo ya wanyama na mafuta ya nazi yalisemekana ni mabaya na yakahusishwa na magonjwa ya moyo. Na nini hasa tafiti za sasa zinasema kuhusu magonjwa ya moyo na aina ya mafuta. 
Soma Jinsi gani kuna utafiti wa kutosha mafuta ya mbegu za mimea sio salama kwa matumizi ya kukaangia chakula na yanaweza kukuhatarisha na magonjwa ya mashambulizi ya mwili kama Pumu,Baridi yabisi,Magonjwa ya moyo na Hata kuongezeka uzito na mvurugiko wa homoni. 
Yaweza kuwa umechanganyikiwa sasa, Ila nakuomba usome kwanza hapa elimu ya sayansi ya mafuta ili ujue misingi ya kibaolojia juu ya vyakula vya mafuta na jinsi gani mwili una ratibu matumizi yake. 
REJEA ZA SOMO HILI (REFERENCES)
[1] “Coconut Oil Is ‘Pure Poison’, Says Harvard Professor | Food | The Guardian,” accessed October 18, 2018, https://www.theguardian.com/food/2018/aug/22/coconut-oil-is-pure-poison-says-harvard-professor.
[2] “2015-2020 Dietary Guidelines – Health.Gov,” accessed October 18, 2018, https://health.gov/dietaryguidelines/2015/guidelines/.
[3] “Randomised Trial of Coconut Oil, Olive Oil or Butter on Blood Lipids and Other Cardiovascular Risk Factors in Healthy Men and Women | BMJ Open,” accessed October 18, 2018, https://bmjopen.bmj.com/node/133027.full.
[4] “Lack of an Association or an Inverse Association between Low-Density-Lipoprotein Cholesterol and Mortality in the Elderly: A Systematic Review | BMJ Open,” accessed October 18, 2018, https://bmjopen.bmj.com/content/6/6/e010401.
[5] Zoë Harcombe et al., “Evidence from Randomised Controlled Trials Did Not Support the Introduction of Dietary Fat Guidelines in 1977 and 1983: A Systematic Review and Meta-Analysis,” Open Heart 2, no. 1 (January 1, 2015): e000196, https://doi.org/10.1136/openhrt-2014-000196.
[6] Zoë Harcombe, Julien S. Baker, and Bruce Davies, “Evidence from Prospective Cohort Studies Did Not Support the Introduction of Dietary Fat Guidelines in 1977 and 1983: A Systematic Review,” Br J Sports Med 51, no. 24 (December 1, 2017): 1737–42, https://doi.org/10.1136/bjsports-2016-096409.
[7] Zoë Harcombe, Julien S. Baker, and Bruce Davies, “Evidence from Prospective Cohort Studies Does Not Support Current Dietary Fat Guidelines: A Systematic Review and Meta-Analysis,” Br J Sports Med 51, no. 24 (December 1, 2017): 1743–49, https://doi.org/10.1136/bjsports-2016-096550.
[8] “The Scientific Report Guiding the US Dietary Guidelines: Is It Scientific? | The BMJ,” accessed October 18, 2018, https://www.bmj.com/content/351/bmj.h4962.
Dr john Masawe
Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?| Founder, CEO and Publisher @wahabarishaji

Latest news

TANESCO yaboresha hali ya umeme Uru Kilimanjaro

 Shirika la umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea na uboreshaji hali ya upatikanaji wa umeme (voltage improvement) maeneo mbalimbali nchini ikiwemo...

Qatar yapinga madai ya kuiunga mkono Israel

Katika mfumo wa maazimio ya kimataifa, Qatar imethibitisha msimamo wake thabiti wa kukomesha uvamizi wa Israeli kwa ardhi ya...

NTV Visits Viral Kids Impersonating Their Anchors [VIDEO]

They say that all it takes to stand out is unique content and as it looks, H-Town Kids, popular...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you