Kangi Lugola na wenzake wahojiwa na TAKUKURU Dodoma

0
5

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya ndani ya Nchi, na Mbunge wa Mwibara, Mhe. Kangi Lugola leo Januari 31, 2020, amehojiwa kwa saa sita na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa nchini (TAKUKURU)  kufuatia agizo la Rais Dk John Magufuli kutaka viongozi hao wahojiwe.

Katika Mahojiano hayo yaliyofanyika Makao Makuu ya TAKUKURU, Jijini Dodoma, ambapo Mhe. Kangi aliwasili Makao Makuu ya Ofisi za Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa nchini (TAKUKURU) Majira ya Saa 7:24 asubuhi na kutoka  saa 12:34 mchana.

Kangi  wenzake watatu ambao ni aliyekuwa Kamishna Jeneral wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi, Jacob Kingu na Naibu Waziri wa Wizara hiyo, Mhandisi Hamad Yusuph Masauni, na aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu Mambo ya ndani Ramadhani Kailima na wote watahojiwa kwa nyakati tofauti.

Wote wanne hao wanahojiwa kufuatia agizo la Rais, Dk.John Magufuli la kuhusu mkataba ilioingiwa na wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi wa Sh Trilioni moja wa vifaa vya Jeshi la Zimamoto.

Advertisements

 Kwa mujibu wa Rais Dk Magufuli hivi karibuni katika hotuba yake alisema mradi huo umesainiwa na kamishna jenerali wa Zimamoto.

Katika kuwasili ofisi hizo ameanza aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani Kangi Lugola,akafuatiwa MA aliyekuwa Katibu wa Wizara ya Mambo ya Ndani Meja Jenerali Jacob Jingu na baadae aliyekuwa Kamishna wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Thobias Andengenye.

Kangi Lugola anakuwa Waziri wa kwanza kutolewa katika nafasi yake na kupelekwa kuhojiwa na Taasisi ya kuzuia na Kupambana na rushwa TAKUKURU, tangu kuanza kwa awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli.

Facebook Comments