Kocha wa Kagera Sugar ajitapa "Nikifunga nafunga kweli"

0
5

MECKY Maxime, Kocha Mkuu wa Kagera Sugar amesema kuwa kilichompa ushindi mbele ya Yanga ni kujiamini na kuiruhusu timu yake icheze bila hofu.

Maxime aliingoza timu yake kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 mbele ya Yanga kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa jana, Januari 15 Uwanja wa Uhuru.

Advertisement

Maxime amesema kuwa hana hofu anapocheza na timu yoyote wakati wowote jambo linalomfanya kupata matokeo na mtego wake ukigundulika anachapwa.

“Kwenye wakati wa kucheza na timu yoyote ninawaruhusu wachezaji kucheza na sio kupaki basi ndio maana ikitokea ninashinda ninafunga kweli na nikibanwa ninafungwa kwa kuwa siruhusu kupaki basi,” amesema.

Ushindi wa mabao 3-0 unaifanya Kagera Sugar kupata ushindi wake wa kwanza ndani ya mwaka 2020 kwani ilipoteza mechi zake zote mbili za mwanzo mwaka huu ilipocheza mbele ya Coastal Union na Polisi Tanzania ikiwa ugenini.

Facebook Comments