LAAC yaitaka Jiji la Dodoma kusimamia kikamilifu Fedha za mikopo ya vikundi vya Halmashauri

0
8

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) imeitaka Halmashauri ya Jiji la Dodoma kusimamia kikamilifu fedha za asilimia kumi 10% ya Mikopo inayotolewa na Halmashauri hiyo kwa makundi Maalamu kwani wamebaini kuwa fedha hizo kutolewa katika vikundi maalumu lakini hazina usimamizi mzuri.

Advertisements

Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Vedasto Ngombare Mwiru, akizungumza wakati wa kuhitimisha ziara ya siku mbili ya Kamati hiyo iliyotembelea miradi mbalimbali katika Jiji la Dodoma kuona utekelezaji wake, sambamba na kukagua vikundi hivyo Kama inatija kwa jamii.

Amesema Kamati yake imebaini fedha hizo zinatolewa kikamilifu lakini zinaonekana hazina Usimamizi mzuri hali inayoweza kusababisha fedha hizo kupotea na kutoleta tija kwa Jamii.

” Hapana shaka kamati imepitia miradi yote ya vikundi, hapana shaka tumebaini fedha hizo hinapelekwa, lakini tulichobaini fedha hizo hazina usimamizi zinatolewa tu lakini hazifuatiliwi na kuona Maendeleo ya vikundi hivyo” amesema Ngombare mwiru.

Ameongeza kuwa ” kutokana na mapungufu hayo Kamati kwa Leo haitoi maelekezo yoyote kwa Halmashauri kuhusu hilo, lakini Mbunge litaendelea siku yoyote kabla ya kumaliza shughuri za Mbunge kamati itarudi tena kuangalia utekelezaji wa haya” amesema.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Godwin Kunambi, amesema Kama Jiji watahakikisha wanayatendea kazi mapungufu hayo yaliyoelezwa na Kamati hiyo na yatarekebishwa haraka iwezekanavyo.

“Mhe Mwenyekiti wa kamati sisi Kama Jiji tunafanya vizuri katika kutenga fedha hizi na tunazitoa kwa makundi yote, lakini niihakikishie Kamati yako tukufu mapungufu hayo tutayarekebisha haraka iwezekanavyo”

“Ameongeza kuwa kwa Mpaka Sasa tumeshatenga kiasi cha Bilioni tatu 3.7 kwa ajili ya makundi hayo ya walemavu asilimia 2, Vijana asilimia 4, na akina mama asilimia 4, na zinawasubiri waje kukopa” amesema Kunambi.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, TAMISEMI, anayeshughulikia Afya, Dkt Dorothy Gwajima, amesema mapungufu hayo yatafanyiwa kazi na kitengo kinachosimamia mikopo hiyo, ambapo kwa niaba ya Katibu Mkuu, ameagiza Halmashauri zote kufuatilia na kusimamia fedha za mikopo hiyo.

Facebook Comments