Maadhimisho ya siku ya Wauguzi Duniani 2020,Kitaifa kufanyika Manyara

0
7

Na John Walter-Manyara

Maadhimisho ya siku ya Wauguzi na wakunga duniani yanayofanyika kila inapofika Mei 12, mwaka 2020 kitaifa yamepangwa kufanyika mjini Babati katika mkoa wa Manyara ambapo mgeni rasmi atakuwa kiongozi mkubwa wa Kitaifa.
Akizungumza na wadau mbalimbali mkoani Manyara,Makamu wa rais wa chama cha wauguzi Tanzania Ibrahim Mgoo, amesema maazimisho haya yataenda sambamba na Jubilei ya miaka 200  tangu kuzaliwa kwa mwasisi wa taaluma hiyo Bi. Florence Ningt Ngale aliezaliwa 12-5-1820 huko nchini Italia .
Amesema katika sherehe hizo,kutahitimishwa kampeni ambayo imekuwa ikiendeshwa tangu January mwaka jana  yenye jina ‘Nursing Now Campaign” ambayo ilikuwa inalenga kuinua hadhi ya Uuguzi duniani,kuonyesha jamii na taasisi zake zote thamani ya kuwepo kwa Taaluma hiyo Muhimu Ulimwenguni.
Katibu Mwenezi msaidizi  wa chama cha wauguzi TANNA Bi.Johari Yusuph, amesema hiyo itakuwa ni nafasi kwa watakaohudhuria kwani mkoa huo una vivutio vingi na ni rahisi kufikika kwa urahisi katika mikoa yote kutokana na Miundo bora ya barabara.
Naye Mganga mkuu wa wa mkoa wa Manyara Dr. Damas Kayera akizungumza na wadau mbalimbali wa Maendeleo mkoani Manyara, amewakaribisha wakunga wote hapa nchini na kuwahakikishia kuwa Mkoa umefanya maandalizi ya  kutosha ili maadhimisho hayo yaweze kufana.
Zaidi ya shilingi milioni 89 zinahitajika ili kuweza kufanikisha hilo, huku watu zaidi 1000 kutoka maeneo mbalimbali ya nchi na nje ya mipaka wakitarajiwa kuhudhuria siku hiyo Muhimu duniani.
Ni mara ya kwanza Kufanyika kwa maadhimisho haya mkoani Manyara,mwaka jana yalifanyika katika mkoa wa Katavi.
Wakazi wa mkoa wa Manyara wanaojishughulisha na utoaji huduma ya vyakula,Usafiri, huduma za kifedha na kulala wageni watanufaika na Maadhimisho hayo kiuchumi.
Aidha huduma mbalimbali za vipimo zitatolewa bure kwa wananchi wote watakaohudhuria siku hiyo.

Facebook Comments