Sport Michezo (Swahili) Maneno ya Ole Gunnar baada ya kumsajili Bruno "Tunahitaji...

Maneno ya Ole Gunnar baada ya kumsajili Bruno “Tunahitaji mchezaji ambaye anaweza kuvunja pua hata kidole chake ili timu ipate matokea”

-

- Advertisment -

Manchester United wamekamilisha saini ya milioni 55 ($ 47m / $ 60m) ya Bruno Fernandes kutoka Sporting, na kiungo huyo akiingia kandarasi ya miaka mitano na nusu huko Old Trafford.

Ole Gunnar Solskjaer aliamua kuimarisha kiungo ya mbele baada ya kupata pigo la viungo wawili kupata majeraha ambao ni Pogba na mctominay. Kufika kwa Fernandes kunapaswa kusaidia kushughulikia mapungufu hayo.

Fernandes aliahidi kutoa mchango wake wote kwa  klabu kabla ya kumshukuru Solskjaer kwa kufunguliwa mlango wa malengo yake, akisema: “Upendo wangu kwa Manchester United ulianza muda  sana wakati nilikuwa nikitazama Cristiano Ronaldo akicheza na tangu wakati huo nimekuwa shabiki mkubwa wa kilabu hii kubwa duniani.

“Kwangu mimi kwa sasa kucheza Manchester United nahisi ni ya maajabu, nimefanya bidii kufikia sasa na ninaweza kuwaahidi mashabiki kuwa nitatoa kila kitu kwa klabu hii nikiwa na jezi hii ili kutusaidia kufanikiwa zaidi. Nataka niishukuru klabu ya Sporting kwa kila kitu walichonifanyia.

“Ni muhimu kusikia maneno mazuri ambayo yamekuwa yakisemwa juu yangu kutoka kwa wachezaji ambao walikuwa wakiichezea timu hii. Asante sana kwa Ole na kila mtu hapa Manchester United kwa imani ambayo wameonyesha kwangu na siwezi kusubiri kuanza kurudisha upendo wao nikiwa uwanjani. “.

Maneno ya Solskjaer, “Tumekuwa tukimfuatilia Bruno kwa miezi mingi na kila mtu hapa amevutiwa sana na sifa zake zote na nini atailetea timu hii,” alisema.

“Muhimu zaidi yeye ni binadamu aliye na utu mkubwa na sifa zake za kuwa kiongozi ziko wazi kwa kila mtu na watu  wanaona.

“Magoli ya Bruno na assists zake kwa wachezaji wengine yanajieleza yenyewe, atakuwa naamini atakuwa msaada mzuri kwa timu yetu na atatusaidia kuendeleza katika sehemu ya pili ya msimu.

Alisema: “Tunahitaji utengenezaji wa magoli mengi , pia tunahitaji magoli mengi zaidi, pia mtu ambaye ataweza hata kuvunja pua au vidole vyake ili timu ipate alama.

“Sio lazima kila wakati tufunge magoli mazuri tu tunchohitaji zaidi ni kutoa changamoto zaidi kwa wapinzani ”

Inaelezwa kuwa United watakuwa na Fernandes mapema leo Ijumaa watakaporejea mazoezini kwa ajili ya mchezo wa Jumamosi ikijiandaa na mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Wolves katika uwanja wa Old Trafford.

By Ally Juma.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Cross River State police commissioner loses mother

Hajia Hajarat Nma Abdulkadir, mother of...

Buhari condoles Umahi, Ebonyi people over death of scores in fatal accident

President Muhammadu Buhari has offered his condolences to the government and people of Ebonyi State over...

Ebonyi : Umahi visits scene of accident, orders immediate investigation

Governor David Umahi of Ebonyi State, on Saturday, visited the Akaeze bridge, the scene of the...

Edo Decides: Police Commission releases report from voting centers

The Police Service Commission (PSC) has...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you