Msemaji wa serikali: Uchumi wa Tanzania umekua kwa 6.9%

0
5

Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amesema kwa takwimu za mpaka September 2019, uchumi wa Tanzania umekua kwa 6.9% huku matarajio yakiwa ni kufikia hadi 7.1% “kwa Afrika Mashariki tunahangaika na Rwanda, kwa Nchi za SADC Tanzania ni miongoni mwa Nchi ambazo zinaongoza kwa uchumi wake kukua kwa kasi” .

“Uchumi unaokua unaweza kuupima kwa namna nyingi mojawapo ni maisha ya Watu, Tanzania ukienda Shule elimu bure, angani kazi zinafanyika, vyuo vikuu ada Wau wanalipiwa, kuakisi kwa uchumi kukua maana yake ni uwezo wa Serikali kufanya mambo mengi” – Dr. Abbas .

“Katika Ripoti ya Transparency 2019 ya January 23, 2020, Tanzania imekuwa ya 96 kutoka ya 117 mwaka 2015 na 103 mwaka 2017, kwa matokeo haya Tanzania ni ya pili kwa Afrika Mashariki kwa kutokuwa na rushwa nyuma ya Rwanda”- Dr. Abbas.

Facebook Comments