Mwakyembe awataka Watanzania waishio nje ya nchi kuwekeza kwenye michezo

0
4

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe.Dkt Harrison Mwakyembe ametoa wito kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi kujitokeza kuchangia ujenzi wa
viwanja vya michezo ambavyo vitasaidia katika kuibua vipaji vya michezo kwa vijana.

Mheshimiwa Mwakyembe ametoa kauli hiyo leo bungeni Jijini Dodoma alipokuwa kijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Viti Maalum Mheshimiwa Cecilia
Pareso (CHADEMA) lilohoji kwanini serikali isijenge Sports Area katika Miji mikubwa kwani kupitia viwanja hivyo kutasaidia kuibua vipaji vingi zaidi kama vya akina
Mbwana Samatta ambao watalitangaza taifa vyema.

Advertisements

‘’Suala la kujenga viwanja vya michezo si la serikali pekee ni pamoja na wadau wote na kwa sasa kuna mtanzania mmoja aishie Marekani ambaye amejenga
uwanja wa michezo mzuri Mkoani Arusha katika eneo la Sekei ambao kwa sasa umekwisha fikia asilimia 90, pia Ofisi ya Halmashauri ya Jiji la Arusha nayo imejenga Sports Arena katika eneo la Ngarenaro hizi zote ni jitihada mbalimbali za kukuza sekta ya michezo na kuibua vipaji,’’alisema Dkt.Mwakyembe.

Swali hilo liliibuka baada ya Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mheshimiwa Juliana Shonza kutoa mjibu ya swali la msingi la Mbunge wa Kinondoni Mhe.Maulid Said Mtulia (CCM) lilohoji serikali inampango gani katika kuimarisha sekta ya michezo kwa kuandaa wakufunzi wa michezo,kujenga viwanja vya
kisasa,kuhakikisha upatikanaji wa vifaa vya michezo ambapo Naibu waziri huyo alijibu kuwa serikali kupitia Chuo cha Michezo Malya kilichopo Mkoani Mwanza
kinatoa kozi mbalimbali katika ngazi ya Stashahada, Diploma in Sport Administration and Couching ambayo hutolewa kwa miaka miwili.

‘’Katika kuimairisha sekta ya michezo serikali imeendelea kutoa mafunzo mbalimbali yanayohusu taaluma tofauti za michezo kupitia Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na elimu ya michezo hutolewa katika ngazi ya Shahada kupitia Idara
Maalumu ya Physical Education and Sports Science (PESS),’’alisema Mhe.Shonza.

Pamoja na hayo Mheshimiwa Shonza aliendelea kusisitiza kuwa suala la ujenzi wa miundombinu ya viwanja si la wizara peke yake nilawatanzania wote ikiwemo
sekta binafsi pia katika kuhakikisha upatikanaji rahisi wa vifaa vya michezo serikali imekuwa ikihamasisha wadau mbalimbali kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya
vifaa vya michezo pamoja wafanyabiashara kuleta vifaaa vya michezo nchini ilikurahisisha upatikanaji wa vifaa hivyo.

Facebook Comments