“Nawapa saa 48 Umeme uwe umeunganishwa hapa”- Dkt. Gwajima

0
13

Naibu Katibu Mkuu OR-TAMISEMI, Dkt. Dorothy Gwajima, ameutaka uongozi wa HalmasHauri ya Nanyamba mkoani Mtwara, kuhakikisha inaunganisha umeme katika chumba cha upasuaji cha kituo cha afya Dinyecha ambacho kinategemewa na wananchi takribani 20,000 waishio katika eneo hilo.

Dkt. Gwajima ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake kufuatia kutokuwepo kwa huduma za upasuaji za uhakika katika kituo hicho zinazo sababishwa na kutegemea umeme wa jenereta ambalo katika siku aliyofika kwa ajili ziara alikuta jenereta hilo limeharibika na hivyo kukwamisha shughuli za upasuaji na shughuli zingine za kitabibu kituoni hapo

Advertisement

“Mimi naondoka hapa Dinyecha lakini ndani ya saa 48 Mganga Mkuu unitumie picha kuonesha mita imefungwa na umeme umeunganishwa hadi chumba cha upasuaji haiwezekani Kituo hiki ambacho Serikali imewekaza fedha nyingi kwaajili yakuwahudumia wananchi mshindwe kufunga umeme   kwa kisingizio cha kukosa shilingi 900,000”. Alionesha kushangazwa Dkt. Gwajima

Kituo hicho ambacho kimekamilisha zoezi la usambazaji wa nyaya (Wire ring) katika majengo yote ya kituo kimebakiza zoezi la kufungiwa mita na kuunganisha umeme wa gridi ya taifa ili uweze kutumika katika shughuli mbali mbali za kitabibu. 

Akitoa maelezo yake mbele ya Naibu Katibu Mkuu, Mganga Mkuu wa Wilaya hiyo Peter Kyabaroti aliwatupia lawama TANESCO kuwa wamekuwa wakitoa maelekezo machache kwa uongozi wa kituo ndio maana shughuli ya ufungaji umeme ikachelewa hata hivyo lawama hizo zilipingwa vikali na Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Ndugu Osca Ngito, kwa kusema sio kweli linalosemwa na Mganga Mkuu wa Wilaya.

Kufuatia hali hiyo ilimlazimu Dkt. Gwajima kwa niaba ya Serikali kutoa saa 48 umeme uwe umekwisha unganishwa na atumiwe picha za ushahidi wa uwepo wa umeme wa Gridi uwe umefungwa na kisha picha zenye kuonesha umeme umeingia tayari chumba cha upasuaji zitumwe TAMISEMI.

Kituo cha Afya Dinyecha ni moja ya vituo vya awali kabisa vilivyo pokea  milioni 500 kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya afya ambapo kwa maelekezo ya serikali walifanya ujenzi huo kwakutumia mafundi wenyeji Local fundi ambapo kwa sasa kituo hicho kinahudumia watu zaidi ya 20,000.

Facebook Comments