Serikali yachukua tahadhari kuhusu tishio la Nzige

0
5

Kutokana na taarifa za kuwepo kwa tishio la kuvamiwa na nzige wa jangwani hapa nchini serikali imeanza kuchukua tahadhari ya kuratibu upatikanaji wa viuatilifu maalum Zaidi ya lita 7,000 vya kuwadhibiti nzige hao.

Mapema mwishoni mwa mwaka jana 2019 nzige wa jangwani waliripotiwa kushambulia maeneo ya kaskazini mwa nchi jirani ya Kenya wakitokea Eritrea na Ethiopia na kuchukua uelekeo wa kusini takribani kilomita 166 kutoka ulipo mpaka wa nchi hiyo na Uganda.

Advertisements

Serikali ya Tanzania imeanza kuchukua tahadhari ya kuwadhibiti nzige hao endapo wataingia hapa nchini pamoja na visumbufu wengine wakiwamo ndege aina ya kwelea kwelea, viwavi jeshi na nzige wekundu.

Waziri wa kilimo Japhet Hasunga amebainisha kuwa nzige hao wana madhara makubwa kwa mazao ya chakula, mimea na uoto wa asili.

Tahadhari inatolewa kwa wananchi hususani wakulima kutoa taarifa kwa uongozi wa serikali za vijiji endapo watabaini uwepo wa wadudu wasiowafahamu ili wizara itume timu ya wataalam kuwachunguza.

Hii si mara ya kwanza kwa Tanzania kukabiliwa na tishio la uvamizi wa nzige wekundu ambapo miaka ya 1960 walishambulia maeneo kadhaa na hivyo Tanzania kulazimika kujiunga na mashirika mawili ya kukabiliana na nzige.

Facebook Comments