Simba kumenyana na Mbao leo

0
4

SVEN Vanderbroek, Kocha Mkuu wa Simba leo ana kazi mbele ya Mbao FC kwenye mchezo utakaochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Sven anaingia kibaruani akiwa na kumbukumbu ya kupokea kichapo cha bao 1-0 mbele ya Mtibwa Sugar kwenye fainali ya Kombe la Mapinduzi na kulipoteza kombe la kwanza.

Advertisement

Leo Simba itamenyana na Mbao FC majira ya saa 10:00 jioni na kazi kubwa itakuwa kulipa kisasi cha msimu uliopita baada ya kufungwa bao 1-0 msimu uliopita mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Bao pekee lilifungwa na Said Khamis, Jr kwa mkwaju wa penalti na ilisababisha aliyekuwa Kocha Mkuu wa wakati huo, Patrick Aussems, kutupiwa chupa na mashabiki kwenye mchezo wake wa nne ambao alipoteza.

Beki kisiki wa Simba, Pascal Wawa amesema maandalizi yanaendelea kila siku na wanahitaji kuona wanapata matokeo.

Facebook Comments