TAKUKURU wamuhoji Lugola kwa saa 5

0
6

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola ameondoka katika ofisi za taasisi ya kupambana na rushwa (TAKUKURU) baada ya kumaliza  kuhojiwa ambapo aliingia saa 1.24 asubuhi na kutoka saa 6.37.

Lugola amehojiwa kwa kutumia muda tofauti na ulivyopangwa ambapo awali alitakiwa kuhojiwa hadi saa 3:30

Hata hivyo, muda wa Kingu kuhojiwa umesogezwa mbele  kwa kuwa Lugola  alikuwa bado katika chumba cha mahojiano.

Pamoja na Lugola  wengine wanaotarajiwa kuhojiwa na Takukuru leo  Katibu Mkuu wa wizara hiyo, Meja Jenerali Jacob Kingu  , Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Hamadi Masauni na aliyekuwa Kamanda wa Kikosi cha Zimamoto na Uokoaji, Thobias Andengenye.

Facebook Comments