Tanzania na Zambia zasaini makubaliano ya kuimalisha biashara , mpaka wa Zambia

0
7

Na Baraka Messa, Songwe

TANZANIA na Zambia zimesaini makubaliano ya kuimalisha uhusiano wa kibiashara katika mpaka wa nchi hizo uliopo Tunduma wilayani Momba mkoani Songwe kati ya Mamlaka ya mapato Tanzania (TRA)na Mamlaka ya mapato Zambia (ZRA) lengo likiwa ni kukuza uchumi kwa kuondoa vikwazo  vya mlundikano wa magari mpakani na kutatua changamoto ya magendo .

Kamishina mkuu mlaka ya mapato Tanzania (TRA) Edwini Mhede alisema kuwa desemba 13 mwakajana 2019 walikutana na Kamishina mkuu wa mapato Zambia (ZRA) kukubaliana kwa pamoja kuimalisha biashara katika nchi hizo mbili ambapo walikubaliana kutatua changamoto ya magari na malori kukaa muda mrefu mpakani hapo baada ya kutoka bandarini DaresSalaam.

Alisema kutokana na nchi hizo mbili kunufaika na mpaka huo jambo kubwa walilokubaliana kwa pamoja ili kutatua changamoto ya mizigo kukaa muda mrefu na kukwamisha shughuli za biashara kuwa walikubaliana kulasimisha utaratibu wa kubadilishana taarifa ya mizigo ikitoka DaresSlaam tujuea taarifa mpaka unapovuka mpaka Nakonde Zambia.

” Ninayo furaha kubwa kuwaambia kuwa tayari tumeshakamilisha makubaliano ambayo tuliahidiana kukamilisha mwezi huu januari , Sasa tuna mahusiano rasmi katika hili eneo la mpaka wetu ,

Advertisements

Tumeziagiza idara zote  zinazohusika na teknolojia na mawasiliano (TEHAMA) kwa upande wa Nchi zote mbili kuhakikisha ndani ya muda usio zidi miezi miwili kuja na mfumo wenye uwezo wa kusoma taarifa za mizigo na magari yanayotoka bandarini moja kwa moja ili kuziona taarifa  kwa muda mwafaka lengo likiwa ni kuongeza ufanisi na kutatua changamoto ya upotevu wa Mapato ” alisema Mhede.

Mhede alisema awali kabla ya ujenzi wa kituo cha forodha katika mpaka wa Tanzania na Zambia Tunduma ufanisi wa  kazi ulikuwa duni kwa kiasi kikubwa ukilinganisha na sasa ambapo ushirikiano umeongezeka na mapato kwa nchi zote yameongezeka kutokana na kupunguza magendo.

Kwa upande wake Kamishina mkuu wa mapato Zambia (ZRA) Kingsley Chanda alisema malengo waliopanga katika nchi hizi mbili tayari yametimia na kudai kuwa ushirikiano mkubwa ndio umepelekea kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika kuboresha mpaka huo ambao ni lango kubwa lanchi za kusini mwa A frika zilizopo Jumuiya (SADC).

Alisema Zambia wataendelea kuboresha na kutatua changamoto ambazo zilikuwa zikikwamisha magari kuchelewa kuvuka kwa kuboresha miundo mbinu ya barabara na kujenga sehemu kwa ajili ya kupaki magari yatakayo ondoa msongamano kwa kiasi kikubwa tofauti na ilivyokuwa awali.

“leo tunasaini mkataba wa maelewano kutokana na makubaliano yetu yenye  maslahi makubwa  kwa nchi zetu mbili katika kukuza biashara katika pande zote mbili kupitia mpaka huu wa Tunduma na Nakonde kuenda vizuri tuliyoyaanzisha desemba 13 mwakajana kuenda vizuri sana, tunaamini wafanya biashara na serikali zote zitanufaika kupitia makubaliano haya” alisema Chanda.

Katibu Tawala tawala wilaya ya Momba  Mary Marco akimwakilisha mkuu wa Wilaya ya Momba alisema uchache wa wafanyakazi na changamoto ya Miundombinu ya barabara kwa upande wa Zambia kumekuwa kukipelekea foleni kubwa ya magari kwa upande wa Tunduma Tanzania.

Naye  Mkuu wa Wilaya ya Nakonde Field Simwinga alisema kuwa kwa kuwa maraisi wawili wa Tanzania na Zambia kwa pamoja walikutana na kuanza mahusiano ya kuboresha mpaka huo , kuwa wao kama watendaji watatekeleza makubaliano na kutatua changamoto ambazo awali zilikuwa zinapelekea kupotea kwa mapato na kukwamisha biashara kwa ujumla.

Akiwa ziaran mkoani Songwe Oktoba 5 mwakajana 2019 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dokta John Magufuli na Rais Edgar Lungu wa Zambia walizindua  jengo la forodha kwa upande wa Tanzania na kuahidi kuuboresha mpaka wa Tunduma kwa upande wa Tanzania na Nakonde kwa upande wa Zambia , ambapo ikiwa ni takribani miezi mitatu tu tayari nchi hizi mbili  zimesaini mkataba wa makubaliano Kupitia kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Mamlaka ya Mapato Zambia (ZRA).

Facebook Comments