Waziri mkuu wa Urusi ajiuzulu

0
8

Waziri mkuu wa Urusi Dmitry Medvedev amewasilisha barua yake ya kujiuzulu kwa rais Vladmir Putin leo.

Putin alikutana na Medvedev baada ya rais kutoa hotuba yake kupitia televisheni ya taifa ambamo amependekeza kufanyia mageuzi katiba ili kulipa bunge uwezo wa kumteua waziri mkuu.

Advertisement

Kwa hivi sasa rais ana mamlaka ya kumteua waziri mkuu. Medvedev alinukuliwa akisema kuwa katika muktadha huu ni wazi kwamba , baraza la mawaziri , linapaswa kumpatia rais wa nchi hiyo fursa ya kuchukua hatua zote zinazostahili.

Putin alinukuliwa akimuelekeza Medvedev kuendelea kuwa katika wadhifa wa waziri mkuu hadi pale baraza jipya la mawaziri litakapoundwa.

Putin alisema katika hotuba yake kwa taifa kuwa Medvedev atateuliwa kuwa naibu mkuu wa baraza la taifa la usalama nchini humo. Putin ni mkuu wa baraza hilo.

Facebook Comments