Wizara ya Elimu: Suala udhalilishajina ukatili kwa watoto ni kikwazo kikubwa

0
8

Na Thabit Madai,Zanzibar.

WIZARA ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar imesema kwamba suala  Udhalilishaji na ukatili kwa watoto ni kikwazo kimoja kikubwa kinachowakwaza Wizara ya hiyo katika kuhakikisha wanawapatia watoto hao  Elimu kama inavyostahiki.

Imesema kuwa Watoto wanapofanyiwa vitendo hivyo vya ukatili na udhalilishaji hupelekea kushindwa kuendelea na masomo yao na kuwaharibia mustakabali wao wa baadae.

Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Elimu ya Maandalizi na Msingi Zanzibar, Safia Ali Rijali wakati akizungumza na Mwandishi wetu juu changamoto na mikakati yao   katika kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji kwa wafunzi mashuleni.

Mkurugenzi Safia alisema kwamba kushamiri kwa vitendo hivyo kwa watoto hupelekea watoto walio wengi Nchini kukosa fursa ya kupata Elimu kama inavyostahiki.

Advertisements

Alisema kuwa vitendo vya ukatili na udhalilishaji kwa watoto hao ni chanzo cha kukosekana kwa Amani na utulivu dhidi ya watoto  na kupelekea kushindwa kupata Elimu kama inavyotakiwa.

“Kama munavyofahamu kwamba jukumu na dhima kubwa ya wizara Elimu kuhakisha watoto wetu wanapata elimu, lakini bila Amani, Bila ya utulivu watoto hawawezi kusoma hivyo Masuala haya ya udhalilishaji na ukatili ni ikwazo kinachotukabili sisi kama Wizara ambapo watoto hawa wanashindwa kupata elimu kama inavyotakiwa” Alisema Mkurugenzi Safia.

Alieleza kwamba kwa kipindi cha mwezi miezi sita Januari hadi Juni mwaka Jana  Wizara ya Elimu  ilipokea Jumla ya kesi 30 za udhalilishaji kwa watoto ambapo kesi 10 zilikuwa za liwati,Unguja 4 na Pemba 6.

Pia alieleza  kesi  za Ubakaji zilikuwa 5 ambapo Unguja ilikuwa  kesi 1 na Pemba Kesi 4 pamoja na Kesi za 11 za  Ujauzito kwa wanafunzi hao ambapo Unguja 8 na Pemba 3.

“Hata hivyo Wizara tulipokea Kesi  za Ndoa za mapema ambazo zilikuwa Kesi 2 tu kwa Upande wa Pemba” alieleza Mkurugenzi huyo.

Aidha alifahamisha kuwa Kesi hizo ni zile zilizosimamiwana na kitengo cha  Elimu Jumuishi na Ofisi za Mrajisi Wizara hiyo.

Hata hivyo Mkurugenzi huyo alieleza kuwa katika maeneo ya Shule hali ya Udhalilishaji ipo kwa kiasi kikubwa ambapo imefikia hatua wanafunzi kwa wanafunzi wanafanyiana vitendo hivyo.

“Inaumiza zaidi tulipokwenda kutembelea baadhi ya Shule Unguja na  Pemba na kubaini wanafunzi kwa wanafunzi kufanya vitendo hivyo kama kulawitiana na hata kusagana kwa watoto wa kike” alieleza  Mkurugenzi huyo.

Aliongeza kueleza kwamba kibaya walichokibaini kuona kwamba hadi wanafunzi wadogo ngazi ya chekechea wanashiriki katika vitendo hivyo.

“Ebu tujiulize kama watoto kuanzia Nursery wameanza vitendo hivi je ikifika miaka 20 au 30 mbele tutakuwa na Taifa gani” alisema Mkurugenzi huyo.

Katika maelezo yake aliwashauri wazazi na waenzi Nchini kukaana watoto karibu ili kujua nyendo zao na kudhibiti kufanya Matendo hayo.

Katika hatua nyingine alishauri Serikali kufanya utafiti maalumu ambao utabaini hasa vyanzo vya ushamiri kwavitendo hivi.

“Nitoe ushauri kwa Serikli kufanya Research ili  nini hasa chanzo  mambo haya, kwa nini watu  wanafanya matendo haya na ilianzaje, maana unapotaka kufanya mzizi watatizo itauwa rahisi utatua jambo hili” alisema Mkurugenzi huyo.

Facebook Comments