Azam yawaita mashabiki uwanja wa uhuru kushuhudia burudani

0
4

JAFFARY Maganga, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kesho, Februari 15 Uwanja wa Uhuru kuona burudani kutoka kwa wachezaji wao watakapopambana mbele ya Coastal Union ya Tanga.

Akizungumza na Saleh Jembe, Maganga amesema kuwa wanatambua mchezo utakuwa mgumu ila watapambana kutoa burudani na kucheza mpira mzuri utakaowapa matokeo.

Advertisements

“Tupo vizuri na morali kwa wachezaji ipo sawa, kwa sasa tunawaomba mashabiki waendelee kujitokeza kwa wingi kuipa sapoti timu na kuona burudani na matokeo mazuri, mchezo wetu dhidi ya Coastal Union utakuwa na ushindani mkubwa na mkali,” amesema.

Azam FC ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi  44 na Coastal Union ipo nafasi ya sita ikiwa na pointi 34.

Facebook Comments