Sport Michezo (Swahili) United yamuweka mbali mshambuliaji wake kutoka China kwa hofu...

United yamuweka mbali mshambuliaji wake kutoka China kwa hofu ya ‘CORONA’, ashindwa kufanya mazoezi Carrington

-

Mchezaji mpya wa Manchester United, Odion Ighalo amekuwa mbali na dimba la mazoezi la Mashetani hao wekundu tangu ajiunge na miamba hiyo ya soka kutoka England kufuatia hofu ya virusi vya Corona.

Odion Ighalo is yet to visit Manchester United's training ground due the coronavirus threat

Nyota huyo mwenye umri wa miaka 30, amejiunga na United kwa mkopo akitokea katika klabu ya Shanghai Shenhua ya China mwishoni mwa dirisha la usajili la mwezi Januari na kutua Manchester, Februari 1, 2020.

Ighalo hajacheza mechi ya ushindani tangu Disemba 6, 2019 na kwa sasa amajiweka sawa kuisaidia United kwenye mchezo wa Premier League dhidi ya Chelsea siku ya Jumatatu.

Ingawaje hafanyi mazoezi katika viwanja vya United, lakini Mchezaji huyo wa Kimataifa wa Nigeria amekuwa akijifua vikali kwenye viunga vya National Taekwondo Centre katika jiji la Manchester tangu alipowasili England.

Kwa mujibu wa ‘The Times’, benchi la matibabu la United linaamini uwezekano wa Ighalo kuwa na virus vya Corona ni mdogo, lakini mshambuliaji huyo ameambiwa kutotembelea viwanja vya mazoezi vya Carrington.

Idadi ya vifo kutokana na virusi vya Corona duniani vinakadiriwa kufikia watu 1,350, wakati zaidi ya watu 60,000 wamegunduliwa nchini China.

Hata hivyo kikosi cha kwanza cha Manchester United kilikuwa Hispania kwaajili ya kujifua na Ighalo anataajiwa kujiunga na wenzake siku ya Jumamosi katika viunga vya Carrington wakati kocha Ole Gunnar Solskjaer amethibitisha kuwa Mnigeria huyo atakuwa sehemu ya wachezaji watakao safiri hadi katika jiji la London kuwakabili Chelsea.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Record flow of boat migrants from Algeria to Spain

More than 20 boats arrived on the eastern coast of Spain from western Algeria carrying illegal migrants and refugees...

CEO mpya Simba, Barbara Gonzalez afanya mazungumzo na Rais wa CAF

try{__scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress();}catch(e){setTimeout( function(){ __scrObj= new __superTag(4644);__scrObj.progress(); } , 3000 )};Afisa Mtendaji Mkuu wa Simba SC, Barbara Gonzalez, amekutana...

Iran Coronavirus Death Toll Tops 25,000

- Society/Culture news - “Unfortunately, 175 (coronavirus patients) lost their lives in the past 24 hours and the...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you