Waasi waidungua helikopta ya Syria

0
5

Vikosi vya Uturuki vinavyoungwa mkono na waasi wa Syria, vimeitungua helikopta ya serikali ya Syria magharibi mwa mji wa Aleppo katika mkoa wa Idlib ulio kaskazini magharibi mwa nchi hiyo.

 Kwa mujibu wa shirika la habari la Uturuki la Anadolu, shambulio hilo limejiri wakati vurugu zikiwa zimezidi katika wiki za hivi karibuni na watu wakiyakimbia makaazi yao.

Kwa mujibu wa habari zilizotolewa kwa shirika la habari la Reuters, ndege za Urusi zilikuwa zikilenga maeneo ya vijijini magharibi mwa Aleppo mapema leo Ijumaa, lakini zilirejea mjini baada ya helikopta hiyo kuangushwa.

Shirika linalofuatilia haki za binaadamu nchini Syria linasema Uturuki imetuma wanajeshi wapatao 6,500 na magari 1,900 ya kijeshi kwenye eneo hilo.

Facebook Comments