Health KUVUNJIKA KWA UUME (PENIS FRACTURE)

KUVUNJIKA KWA UUME (PENIS FRACTURE)

-

- Advertisment -

Kwanza kabisa tuelewe kuwa uume hajaundwa na mfupa wowote bali uume umeundwa na Tishu laini Ambazo unapokuwa na hamu ya tendo la ndoa Tishu hizi zinajaa damu ndipo hapo uume unasimama na kuwa mgumu.


UUME UNAVUNJIKA VIPI?
kuvunjika kwa uume ni pale ambapo nyama ngumu au tendoni zinazoshika uume zinachanika kwa nguvu na kuacha uume kama umevunjika.Hii inatokana na uzito au Mgandamizo mkubwa kwenye uume uliosimama.

Mfano wakati wa tendo la ndoa pale mwanamke anapokua juu au mwanaume anapojichua kwa nguvu sana.
tatizo hili pia inaweza kusababisha kuchanika kwa mishipa ya fahamu, mishipa ya damu na hata njia ya mkojo.

dalili za kuvunjika kwa uume..
sauti ya kuvunjika kitu wakati wa tendo la ndoa likiaambatana na maumivu makali, kuvimba kwa uume na uume kulala ghafla ni dalili kuu kwamba uume umevunjika na unahitaji matibabu.

chanzo ni nini?


karibia wagonjwa wote waliofikishwa hospitali walikua wanashiriki tendo la ndoa kabla ya hali hiyo kutokea,
mwanamke anapokua juu ya uume yeye ndio anakua kama kiongozi wa tendo la ndoa na uzito wote wa mwili wake unakua unaishia juu ya uume wa mwanaume husika,  hivyo asipokua makini atajikuta anaukalia vibaya uume na kuuvunja.

vipimo vinavyofanyika..
vipimo vya utrasound na MRI ndio hutumika zaidi kuhakikisha kweli tatizo hili limetokea na kwa kiasi gani tatizo hili limetokea, pia vipimo hivi vitasaidia katika hatua zifuatazo za matibabu.

matibabu yake
upasuaji ndio njia pekee ya kutibu tatizo la kuvunjika kwa uume na mgonjwa huweza kupona kabisa, kutokufanya upasuaji huweza kusababisha maumivu makali wakati wa tendo la ndoa, kuishiwa nguvu za kiume, uume kupinda milele na kadhalika.

Dr john Masawe
Medical Laboratory Scientist (MLS) |Dancer|Software Developer|Multitalented|??|Entrepreneur|Researcher ?| Founder, CEO and Publisher @wahabarishaji

Latest news

Cross River State police commissioner loses mother

Hajia Hajarat Nma Abdulkadir, mother of...

Buhari condoles Umahi, Ebonyi people over death of scores in fatal accident

President Muhammadu Buhari has offered his condolences to the government and people of Ebonyi State over...

Ebonyi : Umahi visits scene of accident, orders immediate investigation

Governor David Umahi of Ebonyi State, on Saturday, visited the Akaeze bridge, the scene of the...

Edo Decides: Police Commission releases report from voting centers

The Police Service Commission (PSC) has...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you