News Tanzania (swahili) Selous Safari yagawa vifaa vya Usafi kwa wananchi wa...

Selous Safari yagawa vifaa vya Usafi kwa wananchi wa Songosongo

-

- Advertisment -

Na Ahmad Mmow, Lindi

Kampuni inayojihusisha na masuala ya utalii ya Selous Safari Company ambayo pia ina makazi yake kisiwani songosongo yajulikanayo kama Funjove. Imegawa vifaa vya kufanyia usafi kwa wananchi wa Songosongo na kufungua mradi mpya kwa jina la we care project (Tunajali) kama sehemu ya kuimarisha sera ya usafi wa mazingira na ulinzi wa pwani zote unaosimamiwa na BMU (Beach management unit).

Hii ni moja ya ahadi iliyotolewa na funjove kwaajili ya kuibadilisha pwani ya Songosongo na kuipa mwonekano mzuri kwaajili ya kusaidia kupokea watalii. Ikiwa pamoja na kusimamia masuala ya ulinzi ili kulinda mazingira ya samaki na na bahari kwa ujumla.

Akizungumza na viongozi pamoja na wananchi wa Songosongo, meneja mkuu wa funjove Ricus Delport amewaomba wananchi washirikiane kwa pamoja ili kutunza mazingira. Pia, amesisitiza kuitangaza sehemu ya njove na kuahidi kuongeza idadi ya watalii kisiwani hapo endapo tu wananchi watakubali kushiriki kusimamia na kubadilisha mazingira ya kisiwa hicho.

Pia, amewashauri wananchi kutafuta upekee ambao utawavutia watalii kufika eneo hilo kwakua anaamini watalii wengi hupenda vitu vya kawaida kama aina za nyumba, chakula na watu wanaoweza kusimulia vizuri mazingira ya kisiwa hiki. ‘Tujifunze kwa wenzetu wamasai, kila watalii wanapofika kaskazini basi wamasai wapo pembeni wanauza shanga, vikoi na wapo makini sana. Ni vizuri tukijifunza kupitia wao’ Ricus Delport.

Akizungumza na Afisa utawala kampuni ya Selous Safari Company Daniel Vela amesema. Moja ya vitu ambavyo kampuni  hufanya ni kuchangia mafuta kwaajili ya ulinzi ili kusimamia sera ya BMU (beach management unit) sera inayotaka usafi na ulinzi kwa pwani zote. Hivyo hunachangia mafuta lita 200 kila mwezi pamoja na laki 5 kwaajili ya kuimarisha ulinzi.

Kaimu mtendaji wa Songosongo  Ulimboka Ndile, akiri kijiji kunufaika na wawekezaji wa funjovi kwakua wamekua wakijikita zaidi kwenye shughuli za kijamii kama kutoa misaada kwenye hospitali na shule.

Pia, Mzee Salum Yusuph ambaye ni mkazi wa songosongo, awaasa wananchi na familia ya wanasongosongo kubadili misaada kuwa sehem ya maendeleo. Asisitiza kuwa, misaada isiishie kupokea tu. Bali kinachopokelewa kifanyiwe kazi yake na usifanyike ujanja mwingine au uvivu ili watoaji wawe na moyo wa kutoa siku zingine.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Cross River State police commissioner loses mother

Hajia Hajarat Nma Abdulkadir, mother of...

Buhari condoles Umahi, Ebonyi people over death of scores in fatal accident

President Muhammadu Buhari has offered his condolences to the government and people of Ebonyi State over...

Ebonyi : Umahi visits scene of accident, orders immediate investigation

Governor David Umahi of Ebonyi State, on Saturday, visited the Akaeze bridge, the scene of the...

Edo Decides: Police Commission releases report from voting centers

The Police Service Commission (PSC) has...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you