News Mwanablogu wa Iran aliyehukumiwa kifo apewa haki ya kukata...

Mwanablogu wa Iran aliyehukumiwa kifo apewa haki ya kukata rufaa

-

Mamlaka nchini Iran zimesema mpinzani mashuhuri na mwanablogu aliyehukumiwa leo kifo, Ruhollah Zam, anayo haki ya kuukatia rufaa uamuzi huo uliotolewa na mahakama ya kimapinduzi mjini Tehran.

Msemaji wa mahakama, Gholam-Hussein Ismaili, amesema kuwa mwanaharakati huyo anaweza kuomba mapitio ya kesi yake na kubatilishwa kwa hukumu hiyo na mahakama ya juu zaidi.

Mahakama ziitwazo za kimapinduzi zimewekwa maalum kwa ajili ya kesi zinazohusu tuhuma za kufanya ujasusi na kutishia usalama wa taifa.

Zam ametiwa hatiani kwa kutumia tovuti yake, Amad News, kusambaza propaganda dhidi ya uongozi wa Iran na kuchochea maandamano dhidi ya utawala, ambapo baadhi ya wakati yaligeuka kuwa ghasia.

Makhsusi kabisa, anatuhumiwa kupinga vikali mapungufu ya kwenye uchaguzi wa uraia wa mwaka 2009, ambayo yalimuwezesha kuchaguliwa tena rais wa wakati huo, Mahmoud Ahmadinejad.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Leave a Reply

Latest news

‘Elegant’ wings are the secret to how birds fly in gusty winds, say scientists

The secret to how birds are able to fly in gusty winds lies in the “elegant mechanics” of their...

Robert Downey Jr defends Chris Pratt following social media criticism

Robert Downey Jr has defended Marvel co-star Chris Pratt after the actor was criticised on social media. A Twitter user...

Stunning late strike gives Man Utd victory over PSG

PSG 1 - 2 Man Utd Marcus Rashford fired Manchester United to another memorable victory at Paris St Germain as Ole Gunnar Solskjaer’s men...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you