News Amnesty International yataka uchunguzi katika mauaji ya mwanamke mjamzito...

Amnesty International yataka uchunguzi katika mauaji ya mwanamke mjamzito nchini Msumbiji

-

- Advertisment -

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limetaka uchunguzi huru ufanyike, kuhusiana na mauaji dhidi ya mwanamke mjamzito, yaliyofanywa na wanaume waliovalia sare za jeshi katika eneo la kaskazini mwa Msumbiji.

Mkanda wa video ulionekana mtandaoni wiki hii, ukiwaonyesha wanaume hao wakimpiga mwanamke waliyemshutumu kuwa muasi, na kisha kummiminia risasi. 

Serikali ya Msumbiji imewatuhumu wanamgambo wa kijihadi kwa mauaji hayo ya kinyama. Waziri wa mambo ya ndani wa Msumbiji Amade Miquidade ameapa kuchunguza kisa hicho, akisema lakini kuwa kilifanywa na waasi waliovaa sare za jeshi la serikali, ili kuuhadaa umma.

 Amnesty International imesema mkanda huo ni ushahidi wa ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaoendeshwa na maafisa wa usalama wa Msumbiji katika jimbo lenye machafuko la Cabo Delgado.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Cross River State police commissioner loses mother

Hajia Hajarat Nma Abdulkadir, mother of...

Buhari condoles Umahi, Ebonyi people over death of scores in fatal accident

President Muhammadu Buhari has offered his condolences to the government and people of Ebonyi State over...

Ebonyi : Umahi visits scene of accident, orders immediate investigation

Governor David Umahi of Ebonyi State, on Saturday, visited the Akaeze bridge, the scene of the...

Edo Decides: Police Commission releases report from voting centers

The Police Service Commission (PSC) has...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you