News CHADEMA yaahidi kuboresha Maslahi ya watumishi

CHADEMA yaahidi kuboresha Maslahi ya watumishi

-

Na John Walter- BABATI

Mgombea mwenza wa Tundu Lissu kwa tiketi ya  Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) Salum Mwalimu, amehaidi kuwawekea mazingira mazuri wafanyabiashara wote.

Alitoa ahadi hiyo jana Mjini Babati Mkoa wa Manyara  wakati akiwahutubia wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Motel Papaa.

“Suala la kukadiliwa kodi kwa macho ni marufuku na maofisa wa TRA wengine hawajawahi kumiliki hata kibanda cha nyanya,”alisema Mwalimu

Aidha alisema mfanyabiashara hawezi kulinda biashara kwa kupigwa nyundo kichwani na maofisa wa bodi wasiokuwa waaminifu.

Mwanasiasa huyo alifafanua kuwa haki za wafanyabiashara zinatakiwa kulindwa kwa kuwa wanatunza kumbukumbu za biashara zao.

Vile vile alisema miaka mitano iliyopita waliumia sana ila wanaogopa kusema ili wasibambikwe kesi za uhujumu uchumi.

Alisema wengi wao wanafungua maduka yao kwa mazoea huku akiwahakikishia  kufurahia kipindi cha uongozi wa Tundu Lissu.

Alitumia fursa hiyo kumuombea kura Lissu, wabunge na madiwani wa upinzani hasa wa Chadema.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Iraq journalists covering protests threatened with death 

A number of Iraqi journalists revealed that they had received death threats following their coverage of the protests against...

France MPs condemn UAE, Bahrain, Israel normalisation deals

A group of 61 French members of parliament said the ‘peace deals’ signed between Gulf states the UAE and...

4 Job Opportunities at Solidaridad, Project Officers

Solidaridad is a global civil society organization (CSO) that...

2 Job Opportunities at Solidaridad, Senior Project Officers

 Solidaridad is a global civil society organization (CSO) that...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you