News Chama tawala cha Japan chamchagua Suga kama Kiongozi wake...

Chama tawala cha Japan chamchagua Suga kama Kiongozi wake mpya

-

 

Chama tawala cha Japan leo Jumatatu kimemchagua katibu mkuu wa baraza la mawaziri Yoshihide Suga kama kiongozi wake mpya huku kuchaguliwa kwake kukimfanya awe na uhakika wa kuchukua nafasi ya Shinzo Abe kama waziri mkuu wa nchi hiyo.

Suga alishinda kura hiyo kwa urahisi, kwa kupata kura 377 kati ya jumla ya kura 534 kutoka kwa wabunge wa chama cha Liberal Democratic na wawakilishi wa mikoa.Suga aliwashinda kwa mbali Wapinzani wake wakiwemo waziri wa zamani wa ulinzi Shigeru Ishiba na mkuu wa sera wa chama cha LDP Fumio Kishida.

Kwa kuzingatia idadi kubwa ya wabunge wa LDP, Suga pia anatarajiwa kushinda kura ya bunge Jumatano na kuwa waziri mkuu, akichukua nafasi ya Abe, ambaye anajiuzulu kwa sababu za kiafya.

Suga mwenye umri wa miaka 71 ambaye pia ni mshauri na msemaji wa serikali, anaonekana kuwa mtu atakaehakikisha utulivu na muendelezo wa sera za waziri mkuu anaeondoka Shinzo Abe.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Persepolis Loses to Al-Duhail in ACL 2020

- Sports news - Persepolis entered the Matchday Five fixture knowing a win would keep the team top...

39 Job Opportunities at MDH, HIV Testers

HIV Testers 39 PostsManagement and Development for Health (MDH)...

11 Job Opportunities at MDH, Facility Based Trackers

Facility Based Trackers (11 Posts)  Management and Development for Health...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you