News Iran yaionya Marekani dhidi ya kosa la kimkakati baada...

Iran yaionya Marekani dhidi ya kosa la kimkakati baada ya kitisho cha Trump

-

 Iran imeionya Marekani leo dhidi ya kufanya makosa ya kimkakati, baada ya rais Donald Trump kuitishia Tehran, kuhusiana na ripoti kwamba inapanga kulipiza kisasi mauaji ya jenerali wake wa juu Qasem Soleimani.

Msemaji wa serikali ya Iran Ali Rabiei amesema katika mkutano na waandishi habari uliotangazwa kupitia televisheni, kwamba wanatumai Marekani haitafaya makosa hayo na iwapo watayafanya, watashuhudia majibu thabiti ya Iran.

Trump aliapa jana kwamba shambulizi lolote la Iran litakabiliwa na majibu ambayo ukubwa wake utakuwa mara 1,000 zaidi, baada ya ripoti kwamba Iran inapanga kulipa kisasi cha mauaji ya jenerali Qasem Soleimani.

Ripoti ya vyombo vya habari nchini Marekani, ikinukuu maafisa ambao hawakutajwa majina, ilisema mpango wa Iran kumuuwa balozi wa Marekani nchini Afrika Kusini ulikuwa unasukwa kuelekea uchaguzi wa rais wa Marekani mwezi Novemba.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Iraq journalists covering protests threatened with death 

A number of Iraqi journalists revealed that they had received death threats following their coverage of the protests against...

France MPs condemn UAE, Bahrain, Israel normalisation deals

A group of 61 French members of parliament said the ‘peace deals’ signed between Gulf states the UAE and...

4 Job Opportunities at Solidaridad, Project Officers

Solidaridad is a global civil society organization (CSO) that...

2 Job Opportunities at Solidaridad, Senior Project Officers

 Solidaridad is a global civil society organization (CSO) that...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you