News Jimbo la Kaduna laidhinisha sheria ya kuwahasi wabakaji watoto

Jimbo la Kaduna laidhinisha sheria ya kuwahasi wabakaji watoto

-

Kumekuwa na malalamiko makubwa juu ya ubakaji kote nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuniImage caption: Kumekuwa na malalamiko makubwa juu ya ubakaji kote nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni

Gavana wa jimbo la kaskazini magharibi mwa Nigeria la Kaduna, Nasir Ahmad el-Rufai, amesaini sheria inayotoa adhabu kali kwa wanaopatikana na hatia ya ubakaji wa watoto.

Kulingana na sheria hiyo wanaopatikana na hatia ya ubakaji wa watoto walio chini ya umri wa miaka 14 watapewa hukumu ya kufanyiwa upasuaji wa kuwahasi na kifo

Pale ambapo muathiriwa atakuwa na umri wa zaidi ya miaka 14, sharia inasema muhalifu atahukumiwakuhasiwa na kifungo cha maisha.

Wahalifu wa kike watu wazima watakaopatikana na hatia ya kuwabaka watoto watahukumiwa kuondolewa mishipa ya uzazi (fallopian tubes) na kifo.

Katika kesi za ubakaji ambapomuathiriwa ana umri wa miaka 14 , ripoti ya kimatibabu itakuwa muhimu katika kuthibitisha madai.

Wabakaji wa watoto pia wataorodheshwa katika kumbukumbu ya watu wenye makossa ya ngono itakayochapishwa katika vyombo vya habari.

Gavana wa Kaduna alithibitisha kuwa amesaini sheria hiyo katika tweet aliyoituma Jumatano jioni.

Wabunge wa jimbo hilo waliidhinisha muswada wa sharia hiyo wiki iliyopita.

Kaduna ni jimbo pekee nchini Nigeria lenye kipengele cha aina hiyo katika sharia yake ya ubakaji.

Kumekuwa na malalamiko makubwa ya umma dhidi ya ubakajikote nchini Nigeria katika miezi ya hivi karibuni. Licha ya kwamba watu kadhaa wamekuwa wakikamatwa, inaaminiwa kuwa idadi ya wanaopatikana na hatia ni ya chini.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

‘I’m ready to honour police invitation’ – Gbagi reacts to four Delta hotel staff stripped naked

Former Minister of Education (State), Olorogun Kenneth Gbagi, on Saturday, reacted to the report that four staff of Signatious...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you