News Kembaki aomba wakina mama kumchagua

Kembaki aomba wakina mama kumchagua

-

Na Timothy Itembe Mara.

Mgombea Ubunge jimbo la Tarime Mjini kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) Michael Kembaki amewaomba wakina mama kumchagua na kuacha kudanganywa na mgombea wa Chama cha Demokeasia na maendeleo CHADEMA,Esther Matiko ambaye wakati akiwa mbunge hakuwaletea maendeleo.

Kembaki alisema kuwa wakina mama wamuchague na atawatua ndoo ya maji kichwani kulingana na sera ya maji inavyosema kuwa maji yatapatikana mita 400 kutoka wanapokaa.

Kembaki aliongeza kuwa wakina mama wasifanye makosa kama kipindi kilichopita ambapo walimchagua mgombea ubunge wa upinzani na akawaacha kutowafanyia maendeleo na maendeleo yamekwama kuwafikia wakazi wa  jimbo la halmashauri ya Tarime mjini .

“Nimekuwa nanyi kwa kila mnachonituma kufanyiwa licha ya kuwa sikuwa mbunge nimetekeleza ahadi nilizoahidi kipindi nagombea licha ya kuwa kura hazikutosha  ili kuwa mbunge nimehudhuria msiba mbalimbali nimechangia makanisa na misikiti kwa hali hiyo mkinichagua yaliyobaki nitatimiza muniamini na kunichagua muone makeke yangu”alisema Kembaki.

Kembaki alitumia nafasi hiyo kumuombea kura mgombea urais wa Chama chake,John Pombe Magufuli,mgombea udiwani kata ya Bomani Moseti Gotora ili kwenda kushirikiana katika kuleta maendeleo ndani ya halmashauri ya Tarime mjini.

Naye mgombea udiwani kupitia Chama cha mapinduzi (CCM) kata ya Bomani,Museti Gotora aliwataka wapiga kura kumwamini licha ya kuwa nikijana wamtume atawaletea maendeleo kwakushirikiana na viongozi wengine akiwemo Kembaki.

Gotora aliwaomba wapiga kura kuchagua viongozi wanaotokana na Chama chake cha (CCM) ili kuunda mfumo wa uongozi wa mafiga matatu ndipo maendeleo yatakapowafikia kwa wakati na kuonya kuwa wakichagua kwa kuchanganya maendeleo yatakuja kwa kuchanganya.

Kwa upande wake Mairi Wansaku mfanyabiashara wa mafuta ya peterol aliwaomba wananchi wa Tarime mjini kuchagua viongozi wanaotokana na Chama cha mapinduzi ili kujiletea maendeleo huku akimfagilia Rais Magufuli kuwa ametekeleza miradi mingi humu nchini kwa kutumia fedha za mapato ya ndani.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Iraq journalists covering protests threatened with death 

A number of Iraqi journalists revealed that they had received death threats following their coverage of the protests against...

France MPs condemn UAE, Bahrain, Israel normalisation deals

A group of 61 French members of parliament said the ‘peace deals’ signed between Gulf states the UAE and...

4 Job Opportunities at Solidaridad, Project Officers

Solidaridad is a global civil society organization (CSO) that...

2 Job Opportunities at Solidaridad, Senior Project Officers

 Solidaridad is a global civil society organization (CSO) that...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you