News Kimbunga Sally chapiga majimbo ya Alabama na Florida

Kimbunga Sally chapiga majimbo ya Alabama na Florida

-

- Advertisment -

Kimbunga Sally kimepiga mwambao wa karibu na mpaka baina ya majimbo ya Alabama na Florida Kusini mwa Marekani, kikiambatana na mafuriko na upepo unaokwenda kwa kasi ya km 165 kwa saa. 

Mamia ya watu wamelazimika kuokolewa baada ya nyumba zao kujaa maji. Kimbunga hicho kimesomba maboti yaliyokuwa ufukweni na kuyatupa nchi kavu, na kuangusha miti na kuezua nyumba katika miji ya Pensacola na Mobile. 

Nyumba zipatazo 540,000 za makaazi ya watu na biashara zimeachwa bila umeme katika eneo hilo la kaunti ya Escambia, ambako maafisa wamesema watu 377 wameokolewa kutoka nyumba zilizofurika maji, ikiwemo familia ya watu wanne ambao walikuwa wamepanda mitini kuepuka kumezwa na mafuriko.

 Hali ya hatari imetangazwa katika baadhi ya miji ya mwambao katika jimbo la Alabama, wakati vikosi vya kitaifa vya uokozi vikisubiriwa kuwasili katika majimbo yaliyoathiriwa.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

KMC kuivaa Mwadui kesho uwanja wa Mwadui Complex

 Kikosi cha Timu ya  ya Manispaa ya Kinondoni, KMC FC kimejiandaa vilivyo katika  kukabiliana na mchezo wake wa kesho...

US’ Maximum Isolation Outcome of Pressures against Iran: Rouhani

- Politics news - The United States’ legal and political pressures only turned out to be causing maximum...

Citizen TV Responds After OJ Rant Over Tahidi High Episodes

Citizen TV station has responded to former Tahidi High actor Dennis Mugo (popularly OJ) following his outburst around reruns of the...

Tractor Target Beitashour Joins Colorado Rapids

- Sports news - The 33-year-old player has joined Rapids until the end of the 2020 season with...

Lebanese patriarch points at Shia leaders for cabinet delay

Lebanon’s top Christian cleric took a swipe at leaders of the Shia Muslim community on Sunday for making demands...

Ditopile azindua kampeni za udiwani Kibaigwa, "Magufuli kawarahisishia kazi Bodaboda

 Kampeni za Udiwani Kata ya Kibaigwa mkoani Dodoma CCM, zimezinduliwa na Mgombea Ubunge wa Viti Maalum Wanawake Mkoa huo,...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you