News Korti ya Katiba Ivory Coast yamruhusu Rais Ouattara kugombea...

Korti ya Katiba Ivory Coast yamruhusu Rais Ouattara kugombea muhula wa tatu

-

Mahakama ya katiba ya Ivory Coast imemsafishia njia rais wa nchi hiyo Alassane Ouattara kugombea muhula wa tatu. 

Uamuzi huo umefuatiwa na maandamano yenye ghasia, yanayotishia kuitumbukiza nchi hiyo ya Afrika magharibi katika machafuko mithili ya yale ya muongo mmoja uliopita, ambayo yaliangamiza maisha ya watu zaidi ya 3000. 

Aidha, mahakama hiyo hiyo imemzuia rais wa zamani Laurent Gbagbo, na kiongozi wa zamani wa waasi Guillaume Soro kugombea urais katika uchaguzi ujao. 

Majaji wa mahakama hiyo wameridhia wagombea wanne tu kati ya 44 waliotia nia ya kuwania urais katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba 31. 

Miongoni mwa walioruhusiwa kusimama dhidi ya Ouattara no Konan Bedie, rais wa zamani wa Ivory Coast ambaye sasa anao umri wa miaka 86. 

Waandamanaji wenye hasira walichoma magari katika miji ya Yopougon na Bangolo, kufuatia makabiliano baina ya wafuasi wa upinzani na maafisa wa usalama.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Saudi dissidents form pro-democracy political group

A group of Saudi dissidents, most of them in exile, on Wednesday announced the formation of a party to...

Kogi: FCT Minister reacts to death of 23 persons in Lokoja tanker explosion

The FCT Minister of State, Ramatu Aliyu, has reacted to the Kogi State tanker explosion, which claimed the lives...

Insecurity: CISS faults report on Nigeria’s terrorism index

A recent report which ranked Nigeria...

Violence mounts against Iraqi doctors as COVID cases spike

Iraqi doctor Tariq Al-Sheibani remembers little else beyond cowering on the ground as a dozen relatives of a patient,...

Buhari reacts as tanker explosion kills 23 in Kogi

President Muhammadu Buhari has mourned the death of 23 Nigerians in the Kogi State tanker explosion on Wednesday. Muhabarishaji reported...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you