News Lipumba: "Unaweza kumwamkia mtu kumbe ni kijana"

Lipumba: "Unaweza kumwamkia mtu kumbe ni kijana"

-

- Advertisment -

Mgombea Urais kupitia Chama cha Wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba, amesema kuwa, endapo Watanzania watakipa chama hicho ridhaa ya kuongoza nchi kitawekeza kwenye rasilimali watu ikiwemo afya na elimu, ili kuondokana na janga la umaskini.

Lipumba ametoa kauli hiyo hii leo Septemba 13, 2020,  wakati akizungumza kwenye mkutano wake wa kampeni mkoani Iringa, na kuongeza kuwa hali ngumu ya maisha imewafanya vijana kuonekana wazee ili hali umri wao wa kuzeeka haujafika.

“Ukiwapa CCM miaka mitano mingine hivyo vyuma si ndiyo vitatumaliza kabisa, kama hivi sasa vijana wa Ilula mnazeeka kabla ya wakati wenu unaweza ukaja hapa ukamwamkia mtu shikamoo kumbe ni kijana wa juzi bakora za CCM zimemchanganya, kila mtu yupo hoi bin taabani na ndugu zangu bakora za ccm hazina ubaguzi”, amesema Profesa Lipumba

“Tunaomba kura zenu ili biashara zitoke na wananchi waweze kufanya biashara, uwekezaji uongezeke vitunguu vipate soko sio tu Tanzania mpaka Afrika Mashariki yote, watu wapewe utaalamu wa kuweza kuongeza tija katika shughuli zao za kilimo”, ameongeza Profesa Lipumba

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Kenyans, Tanzanians to Reap Ksh33B Windfall from US Govt

Over 4,000 Kenyans are set to benefit from a Ksh33 billion compensation facilitated by the US government.US Secretary of State...

TAMISEMI Deadline Extended for Government Teachers’ Jobs Application

Overview:Regional Governments and Local Authorities are a full ministry...

US Military Tankers Smuggle Oil from Syria to Iraq: Sources

- World news - Local sources, requesting not to be named, told Syria’s official news agency SANA that...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you