News Makusanyo ya michango ya wanachama NSSF yapaa baada ya...

Makusanyo ya michango ya wanachama NSSF yapaa baada ya kuanza kutumia mfumo wa GePG

-

 

Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Mkurugenzi Mkuu wa mfuko wa hifadhi ya Jamii NSSF Bwana William Urio amesema makusanyo ya michango ya wanachama wa mfuko huo yameongezeka mara dufu mara baada ya kuanza kutumia mfumo wa GePG katika taasisi mbalimbali za kiserikali.

Urio ameyasema hayo Jijini Dodoma wakati wa mkutano wa kupokea taarifa ya matokeo ya matumizi na tathmini ya matumizi ya mfumo huo amesema mara baada ya kujiunga na mfumo huo makusanyo yamekuwa yakiongezeka taofauti na hapo mwanzo.

” Mfumo huu umetusaidia sana katika kuongeza makusanyo hata mapato yetu yameongezeka kutoka bilioni 694 kwa mwaka hadi kufikia juni mwaka huu tumefikisha makusanyo tilioni 1.1 hili ni ongezeko kubwa Sana” amesema Bw. Urio.

Amesema kutokana na kujiunga na mfumo huo kumesaidia hata kukua kwa thamani ya mfuko huo ambapo awali mfuko huo ulikuwa na tilioni 3.2 na umekuwa hadi kufikia tilioni 4.4 na hiyo ni ndani ya miaka miwili tu na kusaidia kutoa huduma bora na kwa wakati.

Amesema matumizi ya mfumo huo yamesaidia kuondoa cheki hewa za malipo ambapo kwa kipindi cha awali kulikuwa na cheki hewa nyingi ambazo zilikuwa zikiondoa weredi wa kazi katika mfuko huo.

Ameongeza kuwa ” kabla ya huu mfumo kulikuwa na akaunti za benki 78 lakini baada ya mfumo huu tumeondoa akaunti na kubaki na akaunti 3 tu” amesema.

Amesema kutokana na kuondoa akaunti nyingi kumepunguza makato kutoka milioni 9 hadi kufikia milioni 4 na kumeongeza uwazi Sasa unaweza kujua nini kimeingia na huko mikoani nini kimeingia.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Saudi Arabia seeks Russia’s help to prevent Marib falling into Houthi hands

Saudi Arabia has asked Russia to intervene and help prevent the strategic city of Marib from falling into the...

Sepahan Midfielder Karimi Rues AFC Champions League Exit

- Sports news - The result meant Sepahan joined Al-Ain as the two sides exiting the tournament from...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you