Sport Michezo (Swahili) Mason Greenwood aungana na Phil Foden kuomba msamaha kwa...

Mason Greenwood aungana na Phil Foden kuomba msamaha kwa kosa la kuingiza wanawake kambi ya timu ya taifa

-

- Advertisment -

Mshambuliaji wa kikosi cha England Mason Greenwood amesema ” yeye mwenyewe ndiye wa kulaumiwa” baada ya kuondoshwa kwa kosa la kukiuka muongozo wa karantini kutokana na virusi vya corona huko Iceland.

Mchezaji huyo wa Manchester United na Kiungo wa kati wa Manchester City Phil Foden, waliamriwa kuondoka kwenye kikosi hicho cha Gareth Southgate siku ya Jumatatu.

Greenwood alisema: “Ninaweza tu kuomba msamaha kwa aibu niliyoisababisha.”

Aliongeza: ”Hususani , ninataka kumuomba radhi Gareth Southgate , kwa kumuangusha, wakati alionesha kuniamini kwa kiasi kikubwa.

”Kuichezea England ilikuwa moja kati ya nyakati za kujivunia sana katika maisha yangu na ni mimi pekee ninayepaswa kulaumiwa kwa kosa hili kubwa.

”Ninaiahidi familia yangu, mashabiki, Manchester United na England kuwa hili ni somo nitajifunza.”

Kwa mujibu wa ripoti za Iceland na vyombo vingine, Foden na Greenwood walidaiwa kukutana na wanawake wawili katika sehemu tofauti za hoteli mbali na mahali kikosi cha England kilipokuwa kinakaa.

Southgate amewaelezea wachezaji hao kuwa ‘wajinga’ akiongeza kuwa : ”ni suala kubwa sana na tumelishughulikia namna hiyo na tumechukua hatua haraka sana kadiri tulivyoweza”.

”Tumelishughulikia ipasavyo. Ninatambua umri wao lakini dunia nzima inashughulika na janga hili.”

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Several bandits killed as troops raid Kaduna forest

The Defence Headquarters on Friday said the Air Component of Operation Thunder Strike destroyed bandits’ meeting...

Abia: Ikpeazu has done well – Ngwa Patriots Forum

The president of Apex Ngwa Socio-Political...

French Christian group allegedly backs Syrian regime

A France-based Christian group has allegedly been supporting a militia in Syria loyal to the Bashar al-Assad regime and...

Marekani kupiga marufuku TikTok na WeChat

TikTok na WeChat zitapigwa marufuku nchini Marekani kuanzia Jumapili, endapo Rais Donald Trump atakubali kutekeleza mkataba wa dakika za...

RC Ndikilo atembelea kiwanda cha kisasa cha kuunganishia magari cha GFA Kibaha

 Serikali mkoani Pwani imewataka wawekezaji mbali mbali wa ujenzi wa viwanda kuhakikisha kwamba wanazingatia sheria na taratibu zote zilizowekwa...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you