News Matiko azidi kujinadi kuomba kura

Matiko azidi kujinadi kuomba kura

-

 

    

   Na Timothy Itembe Mara

    MGOMBEA Ubunge Jimbo la Tarime Mjini Esther Matiko azidi kuchanja mbuga huku akiomba wananchi kumchagua na kumpa kura zitakazo mpa ridhaa ya kwenda bungeni ili kuwawakilisha kwa mara nyingine.

    Matiko alibainisha hayo jana kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya mtaa wa Sabasaba mjini hapo ambapo alisema kuwa wananchi wa Tarime hana wasiwasi wataenda kumchagua kuwa mwakilishi wao kwa mara nyingine kwasababu ameshirikiana nao vizuri kipindi kilichopita akiwa mbunge.

    “Wananchi wangu nawapenda najua hamtaniangusha mtanipe kura za kutosha kwa sababu nimeshirikiana nanyi vyema katik shuguli za maendeleo kama vile kuchimba visima vinne,mradi wa maji wa bilion1 ambao ukianza mitaa yote 81 ya Tarime Mjini itanufaika na mradi huo ikiwemo miradi ya elimu na Afya”alisema Matiko.

    Matiko aliongeza kuwa mafanikio hayo hayakuja bure bali walishirikiana na halmashauri ya mjini wa Tarime,kupitia madiwani wakiongozwa na mwenyekiti wake Hamis Nyanswi.

    Mgombea huyo alitumia nafasi hiyo kulaani baadhi ya watu wanaotembea huku wakiendekeza mila potofu kuwa  halmashauri ya Tarime mjini inatawaliwa na mwanamke licha ya kuwa hata Rais Magufuli mwenyewe alisha wahi kusema kuwa wanawake wakipewa nafasi wanaweza.

    Matiko alitumia nafasi hiyo kuwatuliza wananchi wa mtaa wa Sabasaba kuwa wapole wakati Tume ikiendelea kusikiliza rufaa ya wagombea wao ambao waliwekewa pingamizi akiwemo,Pamba Chacha mgombea udiwani kupitia Chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA)na Bashiri Selemani maarufu (SAUTI)na kuwa wasiwe na wasiwasi rufaa yaoitarudi na watakuwa wagombea.

    Kwa upande wake,Teckra Johganes aliwataka wanannchi na wakazi wa Sabasaba kuendelea kuwa na imani na Chadema na wamchague Esther Matiko kwa maendeleo ya Tarime mjini.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

JOHESU calls off nationwide warning strike

A seven-day warning strike embarked upon...

Sudan yataka kuondolewa katika orodha ya wafadhili wa ugaidi

Kiongozi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-BurhanImage caption: Kiongozi wa Sudan, Jenerali Abdel Fattah al-BurhanSudan imetuma ujumbe wa kiwango...

Iran’s Zarif Urges Trump to Rein in Pompeo

- Politics news - “The world says NO Security Council sanctions were restored. But Mr. 'We lied, We...

Former NTV ‘The Trend’ Host James Smart Returns

Former NTV news anchor James Smart on Monday, September 21, announced his return to Nation Media Group (NMG) with...

Esteghlal, Al Shorta Share the Spoils

- Sports news - Al-Ahli of Saudi Arabia has already booked its place in Round of 16 and...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you