News Merkel anaongoza Umoja wa Ulaya kwa mazungumzo na China...

Merkel anaongoza Umoja wa Ulaya kwa mazungumzo na China ili kupunguza mivutano

-

Kansela wa Ujerumani Angela Merkel, maafisa wa ngazi ya juu wa Umoja wa Ulaya pamoja na Rais wa China Xi Jinping wanafanya mazungumzo leo Jumatatu.

Mazungumzo kati ya viongozi hao yamejikita katika masuala ya biashara na uwekezaji na kujenga imani ili kushughulikia masuala magumu ya kisiasa yanayotishia kuharibu uhusiano wao.Merkel, ambaye nchi yake kwa sasa inashikilia Urais wa kupokezana wa Umoja wa Ulaya, atajiunga na Rais wa baraza la Ulaya Charles Michel,

 Rais wa Halmashauri kuu ya Ulaya Ursula von der Leyen na mkuu wa sera ya nje wa umoja huo Josep Borell kwa mkutano wa video ambao umeanza saa sita kamili kwa majira ya Ulaya.

Mazungumzo kati ya China na Ujerumani, nchi zenye uchumi mkubwa duniani, yataruhusu kutathmini uhusiano wao pamoja na nchi nyengine za Ulaya.

Pia mazungumzo hayo yataangazia masuala ya uchumi, mageuzi katika shirika la biashara duniani, mabadiliko ya tabia nchini na janga la virusi vya Corona.

Publisher
Swahili Publisher , Publishes swahili articles in this website

Latest news

Angry Mourners Chase 2 MPs Away From Funeral [VIDEO]

Two lawmakers were, on Saturday, September 26, chased away from a funeral while demanding to give an address.The two;...

Why petroleum marketers will not join planned strike – IPMAN

The National Executive Council of the...

NCC boss, Danbatta, bags prestigious Zik Prize

Prof. Umar Danbatta, the Executive Vice...

Must read

You might also likeRELATED
Recommended to you